Kwa kawaida huwa napenda kusoma matangazo na mabango ya biashara yanayobandikwa sehemu ambapo yanaitaji kusomwa.
Wakati nilipokuwa naliangalia bango lenye tangazo la uvuvi haramu wa kutumia baruti hilo sehemu ya kivuko upande wa Kigamboni, kwani ndilo linalowapokea watu wanaoshuuka katika pantoni nilijikuta najiuliza kama kweli bado ninakikumbuka kiswahili sawasawa.
Nilivyofahamu mimi ni kuwa maandishi mekundu ni kwa kiswahili na ya kijani ni kwa kiingereza, lakini nilipojaribu kutafsiri mwenyewe kila mahali nilijikuta nagonga mwamba.
Hata hilo neno kizazikijazcho sikulielewa, nahisi walitaka kuandika kizazi kijacho, nina wasiwasi hata walioandaa bango hilo walitoa oda maalumu kutoka "China"
Bado najiuliza... hatuna watu wa kuhakiki kinachoandikwa, au wote wamesoma sekondari za kata maarufu kama sekondari za maamuzi magumu!
3 comments:
Lilikuwa dili hilo!
Ila haki ya nani BONGO wala huhitaji MCHINA akuandikie kibao ili kiswahili kikosewe!:-(
Unajua ndio ule uchoyo wa watu, wanataka kila kitu wafanye wao, Directo, editor, mwandishi nk...jamani kila fanii ina mtu wake,na huwezi ukama mkamilifu kwa kila kitu, ndio maana kunakuwa na `wakaguzi' ...mtarfiki, akina nani wale...wote hawo kazi yaO ni kukagua KAZI ZA WENGINE... Kile ulichofanya kuwa kipo sahihi, sawasawa...au sio. Ni bora tupeane kazi...au sio, naona hata mimi ninapoandika, najikuta neno la mbeli limekua nyuma...ni makosa ya kibinadamu, na hayo yataondoka kama utampa mwenzako akusahihishe, wapo wasahihishaji..tuache ubinafsi! TUPO PAMOJA MKUU
ha ha haaaa, hii ni kali ya mwaka
Post a Comment