Member of EVRS

Sunday, 10 July 2011

Yanga Mabingwa wa Cecafa Kagame Cup 2011


Wachezaji wa Yanga wakifurahia ushindi huku wakiwa gizani

Mashabikiwa Yanga wakiwa na furaha baada ya kupata goli

Mashabikiwa Simba wakiwa katika huzuni
 Timu ya mpira wa miguu ya Yanga kutoka Dar es Salaam, Tanzania, imefanikiwa kutwaa ubingwa wa klabu za mpira wa miguu kutoka ukanda wa Afrika Mashariki ambao mwaka huu ulipewa jina la Cecafa Kagame Casttle Cup baada ya kuwalaza wapinzani wao wa jadi Simba SC ya Dar es Salaam pia.
Mpira wa leo ulikuwa mzuri kwa timu zote ukilinganisha na mechi za timu zote mbili wakati zilipocheza nusu fainali, na kila moja kufanikiwa kuingia fainal baada ya kuzitoa timu pinzani zao kwa mikwaju ya penati.
Yanga imepata ushindi wa bao 1 - 0 dhidi ya Simba, bao hili lilifungwa kwa kichwa na mchezajiwa kimataifa kutoka Ghana, Kenneth Asamoah.
Mbali na uzuri wa mechi hii, dosari haikukosekana pale wakati wachezaji wakipewa medali zao, kabla mabingwa wa mwaka huu kupanda jukwaani, umeme ulizimika uwanjani kukawa na giza kabisa, na haukuweza kuwashwa tena. Medali za Yanga zilitolewa kwa msaada wa taa za gari la wagonjwa (Ambulance) ambalo lililazimika kusogea karibu na jukwaa la zawadi ili mgeni rasmi katika pambano hilo atoe medali za dhahabu kwa mabingwa hao wapya wa Cecafa.

Dosari nyingine ilikuwa ni mwandishi wa habari aliyekuwa amevaa fulana ya njano kutimuliwa na polisi asikae karibu na mashabiki wa Simba, na mashabiki wa Yanga walijibu mapigo kwa kuwatimua wahudumu wa msalaba mwekundu waliokuwa wamekaa karibu nao, kwani mavazi yao huwa na rangi nyekendu na nyeupe, ambazo ndizo rangi za klabu ya Simba. Hali hii ikiendelea ni hatari!
Kocha wa Simba Basena alipohojiwa na Supersport, alidai anasikitika kwa timu yake kufungwa na Timu ya kawaida, hii inaashiria ya kuwa Timu ya Simba iliingia kwa kujiamini sana, na matokeo yake ilizidiwa na mwisho kupoteza mchezo.

Picha kutoka Mtaa kwa Mtaa

6 comments:

SIMON KITURURU said...

Hivi katika shindano hili kijina hilo neno Kagame ni kagame Rais au latokea wapi?

Samahani huwa sifuatilii sana mpira kama nifuatiliavyo historia za BIA!:-(

chib said...

Kitururu, Rais Kagame wa Rwanda ndio huwa anatoa pesa za washindi, kama dola 60,000 kila mwaka, ndio maana likapewa jina lake

SIMON KITURURU said...

Hivi Kagame analipwa shilingi ngapi kama Rais ili awe na 60 thau za machejo?

Au ndio mambo ya matumizi ya misaada ya serikali za nje yatumikavyo katika bajeti ya serika yake?

chib said...

Swali gumu hilo Mkuu. Ila nafikiri lipo kwenye bajeti ofisi ya Rais michezo, na huwa anazisaidia sana timu za michezo yote hapa Rwanda

emu-three said...

Nafikiri katika mpira kuna watu wapo radhi wawe masikini kwa ajili ya kusaidia hilo, nafikiri Kagame aliliona hilo, ndio akatoa hilo kombe...sio mbaya, kwani wengi wanafaidikia kw kutumia mgongo wake...
Labda ningeshauri kuwa kungekuwa na kombe la `Wanamapinduzi wa Afrika' watajwe kama Mandela, Nyerere, Kwame..nk, hili lianze kushindaniwa kiafrika, hatimaye litahamasisha na kuikuza historia ya Afrika, eti?

Ivo Serentha and Friends said...

Congratulations on the victory!

True, the images of the ice at the poles will be increasingly restricted