Thursday, 14 July 2011
Rostam Aziz Kujiuzulu Ubunge na Ujumbe wa NEC: Hotuba Kamili
Rostam Aziz, ambaye ni mbunge wa Igunga, au aliyekuwa mbunge wa Igunga kama amekubaliwa kujiuzulu, jana kwnye muda wa saa 7 mchana alitangaza kujiuzulu nafasi zake zote za kisiasa alizozipata akiwa ndani ya CCM na kubakia kuwa mwanachama wa kawaida.
Alitaja sababu nyingi lakini kubwa ni kuwa amechoka na siasa za uchwara na tuhuma zisizo na ushahidi ambazo zimekuwa zikielekezwa kwake kwa muda mrefu.
Hotuba yake kamili inapatikana hapa
Mbali ya kutoa sababu hizo, alijivunia mafanikio aliyoyapata kwa kipindi cha miaka 18 aliyokuwa mbunge, mara baada ya kushinda uchaguzi mdogo kufuatia kifo cha aliyekuwa mbunge wa Igunga Charles Kabeho.
Kuna mabo kadhaa wa kadha yaliyojitokeza katika mkutano huo aliouita wa kuongea na wazee wa Igunga.
Kwangu naona kama alichelewa mno kutoa uamuzi huu, na hivyo kuendelea kupakwa madongo kwa tuhuma mbalimbali alizohusishwa nazo ikiwamo ya kampuni ya kufua umeme ya Richmond na baadaye Dowans (ambayo ilikuwa inasemekana ilikuwa ikitumia anuani ya posta na abarua pepe ya huyu mheshimiwa mstaafu), na pia kuna nyaraka mbalimbali za mawasiliano kati ya Tanesco na Dowans ambazo zilikuwa zinalitaja jina lake katika masuala ya makubaliano katika mktaba tata uliowekwa kati ta ya Tanesco na Dowans.
Ingekuwa busara mheshimiwa huyu angechukua uamuzi wa uwajibikaji kama alivyofanya aliyekuwa mkuu wa IMF au Mzee Mwinyi wakati ule alipokuwa waziri wa mambo ya ndani.
Nina matumaini mwenyekiti wake atakubaliana na uamuzi wa kada huyu ili kujenga imani kwa serikali yake kuwa ni sikivu na inayowajibika kisheria kwa sasa.
Mengi tunawaachia wanasiasa na wanachi waamue....
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
2 comments:
Thanks for visiting, come back whenever you want
Antonio Gallobar
Mambo ya siasa hayo, yetu macho!
Post a Comment