Member of EVRS

Sunday, 24 July 2011

Mauaji ya Norway: Ukatili Dhidi ya Haki ya Kuishi

Anders Behring Breivik (Pichani juu), ambaye ni raia wa Norway ameitikisa dunia wiki hii kwa kufanya mauaji ya kikatili ya karibu watu 100 kwa siku moja katika mji mkuu wa Norway, Oslo. 
  
Sababu kubwa za kufanya mauaji hayo bado zipo kwenye uchunguzi mkali unaofanywa na Serikali ya Norway. Mtu huyu alikamatwa siku hiyohiyo aliyofanya mauaji ya kutisha na kinyama, kwani aliwashambulia kwa risasi vijana waliokuwa katika mkutano wa mafunzo ya kisisasa wanaounga mkono chama kinachotawala Norway. Inadaiwa siku ya kufanya shambulio hilo, alikuwa amevaa nguo kama askari.
Mtu huyu, pia anahusishwa na kutega bomu lililolipuka karibu na ofisi kuu za Serikali mjini Oslo. Siku ya tukio hili la kutisha, maiti 7 zilipatikana karibu na eneo lilipolipuka bomu hilo, na ilikuwa inahofiwa kuwa huenda kuna baadhi ya watu wanaweza kuwa wamefukiwa na kifusi cha jengo lililobomoka kutokana na bomu lililolipuka.  
  
Tukio hili linasikitisha sana, na haieleweki huyu jamaa kama alishirikiana na mtu yeyote, japo alipohojiwa alidai yeye akushirikiana na mtu au kikundo chochote kutekeleza azma yake hii mbaya sana.  
  
Tunaombea amani na utulivu katika nchi ya Norway tukiwa na matumaini ya kuwa tukio kama hili halitarudiwa tena!  

4 comments:

Goodman Manyanya Phiri said...

Huyu jamaa anahitaji uchunguzi mkali wa kisaikolojia. Huenda anaweza akatusaidia sana kama binadamu sisi ili tuelewe ni chombo gani hasa tunaobeba juu ya mabega yetu, kile kinachozungukwa na masikio yaani.

Asante kwa picha, Mkuu; asante kwa kunivutia ili nisome stori la sivyo nilikuwa naikwepa kwa pilikapilika zangu nyingi kortini za huku Afrika Kusini.

Sasa hicho kidevu chake ndio mtindo mpya wa vichaa huko Norway au mimi nimepitwa na wakati? LOL!

emu-three said...

Huyu yeye hawezi kuita GAIDI?

Swahili na Waswahili said...

Mungu wabariki watu Norway na uwaokoe na majanga haya!!!!!

EDNA said...

Dhambi aliyotenda kwa wanorway kamwe haitasahaulika.Cha ajabu wanasema endapo atapatikana na hatia ya hayo mauaji atatumikia miaka 21 jela, WHAT IS 21 YRS? kwa muuaji kama huyu? that means akitoka atakuwa na umri wa miaka 53umri ambao bado atakuwa ni kijana mwenye nguvu zake kufanya uhalifu wa aina yoyote tena,na hebu fikiria wale waliopoteza ndugu zao ,rafiki watoto zao na hata wale walionusurika watakuwa wakimuona akikatiza mitaa bila wasiwasi.Anyway let`s wait and see.