Member of EVRS

Tuesday 19 July 2011

Mzaha kwa Tanesco!

Utani mwingine bwana.....

Ati kwa sababu nyaya za umeme za Tanzania hazipitishi umeme kwa sababu ya mgao, kwa hiyo kwa sasa hazina la kufanya zaidi ya kujitafutia michezo ili kupitisha muda zikishirikiana na nguzo.

Mojawapo ya michezo inazofanya ambayo ni ya kitoto ni kuruka kamba kama unavyoona katika opicha hiyo hapo juu :-)

7 comments:

Anonymous said...

Duh

malkiory matiya said...

Utamaduni wa kujiwajibisha kwa viongozi Tanzania inaelekea ni msamiati. Fikiria suala milipuko ya mabomu, mauaji ya Arusha. Inasikitisha kuona mawaziri husika bado wanadunda.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

wazo hili limekaa kingono ngono zaidi maana lile linapanua miguu na kuruka

Simon Kitururu said...

Nyaya za umeme Tanzania zafaa kweli kuanikia nguo!:-(

DIGITAL WORLD PAGES ARCHIVE said...

This is very unique!

emu-three said...

Ni AIBU...Unajua aibu, hii kwetu kama taifa ni aibu, labda kama wenzangu hawalioni hilo...habu fikirieni wazee wetu walivyojitahidi, mapaka tukaikuta hiyo TANESCO, HIYO TRA, HIYO TTCL, HIYO NANIHII...ina maana sisi hatuna uwezo wa kujiendeleza, habu kwa mafnoo kama isingekuwepo, ina maana sisi sasa tungekuwa gizani...hii kwangu naiona ni aibu, ni kama vile umekuta nyumba ya mzazi wako, wewe unajua kuishi tu, inaanza kubomoka unasema huna uwezo wa kuikarabati...je kama baba yako asingeijenga hiyo ungesihii wapi...hatuna wataalamu, hatuna malighafi...mbona millioni 50 za kila idara zilipatikana chapuchapu...! Labda mimi akili yangu haiwazi wawazavyo wao!
Yaani sasa hivi hakuna cha mgawo tena, ni giza kwa kwenda mbele, umeme unarudi kama dakika tano unaima unarudi tena unazima..hii inatuunguzia vyombo vyetu.
KICHEKESHO: Eti ukiwaka hivyo ni mhusika mkuu wa kuwasha na kuzima anatoa amri kwa vile anataka kunyosha pasi...akimaliza anasema `haya zima haraka'....mkewe akiataka kutoka kwenda kitchenparty anawaambia washeni kidogo...mkewe akimaliza haya zima...lol

Rachel Siwa said...

Hahahhaha nimecheka mpaka basi,kaka wa mimi @Kitururu zinafaa kuanikia nguo,tena zile nguo nyepesi kama mashati ya shule,mataulo,maduveti hazifai!!!!!