Member of EVRS

Wednesday 30 June 2010

Tuepukane na Ufinyu wa Kufikiria

Bado ile habari niliyoiona kwenye runinga juzi iliyohusu watoto wa shule ya msingi huko Mkoani Tanga ya kutokuvaa viatu wakienda shuleni bado inanigonga kichwa!!

Yaani shule nzima ... mwanafunzi mmoja tu ndio alikutwa amevaa viatu, kati ya mamia ya wanafunzi... yaani miguu miwili tu ndio ilikuwa imefunikwa kwa viatu, ha ha haaa, yaani hapo najaribu kuongeza idadi ya kuhesabu, japo nikisema miguu miwili nimevuka moja...

Kikubwa zaidi ni pale msamaria mwema mmoja kutoka Kenya, alipopata habari za awali, ambazo zilitolewa na mwandishi wa habari siku za nyuma, alikuja kutoa msaada wa viatu jozi 50 kwa shule hiyo, kama njia ya kuwasaidia watoto kuvaa viatu.

Yaelekea hilo hilo tatizo ni la siku nyingi, kwani naibu waziri wa masuala ya elimu nk, alikuwa mmoja wa wageni walioenda kupokea msaada huo, alisema wazi ya kuwa mkuu aliyetangulia hapo alikweka sheria ya kuwa wattot wote ni lazima wanunuliwe viatu vya shule, lakini alipohamishwa, viatu navyo vikahama.

Sababu ya kutokuvaa viatu inachekesha, ha ha haaaa...., eti wenyeji wana imani ya kuwa uvaaji wa viatu huleta sugu kwenye miguu, he he heeee
Hivi kipi kinaleta sugu zaidi, kupiga peku au kuvaa viatu viavyokutosha?!

Kuna sehemu za mkoa wa Tanga ni maarufu kwa kuwa na funza wengi, tena wanakula miguu haooo,........ utakuta watoto wadogo miguu imevimba sana, na watu wazima miguu ikiwa imekwenda tenge, mtu anaenda mbele, miguu inaeleekea kulia na kushoto, kiasi kwamba unashindwa kujua anaelekea wapi......

Jamani visingizio visivyo na maana viachwe, watoto wanunuliwe viatu alaaaaaa....

9 comments:

José Ramón said...

Thanks for your visits and your comments and include your blog in my directory of:Various topics.

Collaborating with Blogs Web Creativity and ImaginationA greeting from Spain and keep enjoying the football World Cup

Shukrani kwa ajili ya ziara yako na maoni yako na ni pamoja na blog yako katika orodha yanguMada mbalimbali. Blogs Web kwa ushirikiano na Ubunifu na mawazoA salamu kutoka Hispania na kuendelea kufurahia football World Cup

Anonymous said...

He he heee, mambo ya google translator, raha tupu he he heee

Yasinta Ngonyani said...

Ni jambo la kusikitisha kwa kweli hata kandambili tu inashindikana???

Na kaka Chib naona umefanya mabadiliko katika kibaraza chako. Kinapendeza:-)

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

mimi nilikuwa na viatu wakati nasoma likini sikupenda kuvivaa kwani wenzangu hawakuwa na viatu, ila nadhini ni raha kutembea peku kama mimi mkulima wa bongo

ila sasa, kwenye ulimengu waishia mabishoo kama chib, nasikia aibu na kuamua kuvaa viatu wasinisheke!!!!!!

natamani kutembea peku na kutembea bila ngua, inapunguza gharama za maisha

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

mimi nilikuwa na viatu wakati nasoma likini sikupenda kuvivaa kwani wenzangu hawakuwa na viatu, ila nadhini ni raha kutembea peku kama mimi mkulima wa bongo

ila sasa, kwenye ulimengu waishia mabishoo kama chib, nasikia aibu na kuamua kuvaa viatu wasinisheke!!!!!!

natamani kutembea peku na kutembea bila ngua, inapunguza gharama za maisha

chib said...

@ Kamala, nani kakwambia mie ni bishoo :-)
Watu wa Kanyigo bwana ndio mabishoo namba wani.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

kumbe wa kanyigo mabishoo?? mimi niwa kiziba!!!

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

mjadala mtamu huoooooo!

Haya natusikie bhita kati ya kiziba na Kanyigo mweee!!!!

Kaka Chib, umaskini baba ndo sababu wengine hatuna viatu... :-(

Sasa unashangaa nini kwa mkenya kutuletea viatu? Mbona hukushangaa mr prezidaa alipotembeza bakuli pale Ngurudoto wakati wa wale mafisadi wa Sulivani na wakachanga $100 kila mmoja na prezidaa anachekelea tu?

Haafu si wajua kuwa ile shule ya umasaini ambayo wanakaa chini ilivumbuliwa na wazungu hao na wakachangisha $25,000 za madawati mbele ya prezidaa?

sasa washangaa nini cha ajabu hapo? Au miwani yangu imetoboka? niletee spea mkuu...lol!

chib said...

@ Chacha, umeshinda kaka kwa nguvu ya hoja, na sio hoja ya nguvu