Member of EVRS

Tuesday 15 June 2010

American Lawyer Denied Bail in Rwanda

Prof.Peter Erlinder (in pink prisoner dress) who was arrested in Kigali, Rwanda and charged for genocidal denial through his speeches and publications, has been denied bail out as he requested to be considered in huanitarian grounds, where he is intending to travel to USA for appropriate treatment to his ill/risky healthy conditions as he brought papers showing that he was diagnosed to have brain, skin and heart problems which may turn into cancer.
Read more information in English here

Inadaiwa Mmarekani huyu ambaye pia ni mwanasheria na pia ni profesa, alipoingia Rwanda alikuwa anapinga uwepo wa mauaji ya Kimbari - Rwanda, kimsingi kukana mauaji hayo hapa Rwanda ni kosa la jinai, na ikithibitishwa una imani hiyo, unachukuliwa kama mtu ambaye unachochea mauaji kama hayo na adhabu yake ni kali.

Mzungu huyu anadai alipimwa Marekani na kugundulika ana uvimbe kwenye ubongo, pia ana matatizo ya moyo na ngozi ambayo yanaweza kumsababishia kupata saratani ambayo hata hivyo haikufafanuliwa. Mahakama pia iliambiwa ya kuwa alikuwa kwenye harakati za kuandika historia mpya ya mauaji ya kimbari ya 1994, na kudaiwa kuwa alikuwa anataka kupotosha ukweli wa mauaji hayo.

Mtuhumiwa huyu pia anadai anapata mateso ya kulala ndani ya selo kwa sababu ya kelele za mbu, hivyo analazimika kuweka karatasi ya chooni (toilet paper) masikioni kuziba ili asisikie kelele za mbu!, maana yake kuwa chandarua hakitoshi, bali anataka mbu nao wanyamaze :-)

Hivyo, aliomba aachiwe kwa dhamani ki-ubinadamu ili aende Marekani akapate matibabu sahihi! Nami nafikiri pia aepuke kelele za vuvuzela za mbu wa Rwanda.

Wiki hii shauri lake litasikilizwa tena ili kama atastahili kupewa dhamana.

5 comments:

Subi Nukta said...

Huyu kuku matatizo yake ya akili ni makubwa, kweli ubongo wake kama alivyosema mwenyewe, una matatizo, huenda ndiyo chanzo cha kuongea urojo anaoongea.

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

sasa akijijua chizi ndo aje kufanya uchizi wake rwanda>?? basi na atibiwe rwanda!\


eti kelele za mbu!!! kwanikabla ya kusema alichokisema si alikuwa rwanda?/ mbu hawakuwepo?? mbona hakuwalalamikia na badala yake anawalalamikia baada yakuingia sero??

chib msaidie

chib said...

Ha haa haaa, Kamala kusema ukweli huyu jamaa kachanganyikiwa tu. Kitendo cha kuziba masikio asisikie kelele za mbu ni ushahidi.

Nitashauri apelekwe kwa daktari wa chizis

Anonymous said...

Jamni huyo askari mbona ana tumbo kubwa, Mzungu akiamua kutimua mbio ataweza kumkamata?

Thom said...

This man has been released