Member of EVRS

Tuesday, 29 June 2010

Gari ya Ubalozi wa Tanzania Burundi Yalipuliwa kwa Bomu

Katika harakati za uchaguzi wa urais Burundi jana, watu wasiojulikana walirusha bomu la kutupa kwa mkono mjini Bujumbura na kulipuka na kusababisha kuharibika kwa gari la ubalozi wa Tanzania Burundi. Watu hao walikuwa katika gari ya kiraia walitokomea haraka sana baada ya kurusha bomu hilo.

Hakuna mtu aliyejeruhiwa na hakukuwa na taarifa rasmi kutoka katika ofisi ya ubalozi wa Tanzania mjini Bujumbura.

Kwa kawaida maeneo haya ya maziwa makuu, unapokaribia uchaguzi, visa vya kurusha mabomu ya aina hii hujitokeza hasa Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Inasemekanan mitaa ya Bujumbura jana ilikuwa na watu wachache sana.

Huwa siwaelewi watu wanaosubiri kwenye matukio kama haya kuanzisha vurugu ambazo hazina tija

1 comment:

EDNA said...

wameshaanza mambo yao,sasa wanapata nini wakisha rusha hayo mabomu.