Member of EVRS

Monday, 21 June 2010

Je, Wajua Haya?

Nafikiri wafahamu ya kuwa watu wengi duniani wanatumia zaidi mkono wa kulia kwa shughuli mbalimbali kuliko wa kushoto.

Je unajua ya kuwa watu wengi hupenda kubeba mikoba au mabegi yao katika bega la kushoto?

Na je wajua ya kuwa watu wanapokaa mahali na kusikiliza kitu kwa makini au kuwa katika mawazo fulani, huwa kichwa hakikai wima, yaani hupindisha kidogo shingo yao upande mmojawapo?

Je unajua ni kwa sababu gani?

Kama hujui nakupa mwaka mzima wa kutafakari, mie nitatoa jibu tarehe na mwezi kama wa leo, siku ya Jumanne mwaka kesho.

Nakutakia jumatatu njema

3 comments:

John Mwaipopo said...

which also depends on you still 'being there', you know what i mean.

chib said...

@Mwaipopo, Huku shwari bwana, ninadunda na nitaendelea kudunda ndugu yangu ha ha haaa

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

ni kwa sababu wengi wetu hutumia akili za upandwakushoto na ndio maana watumiao mikono ya kushoto uonekana kuwa na akili sana kwani wanatumia pande zote mbili za akili