This friday.. I want to give you a funny tale, ha haaa haaa
I cant wait, but is a story of a parrot who guide the house from the thief.
Just visit this site to laugh, ha ha haaa
I suffered worthless theft from my house-keeper :-(
Sasa tuache utani, wiki hii yaani imenitia simanzi kabisa, nimeshindwa kuikalia blogu hii kwa sababu ya tukio la wizi, duh!! Polisi wa Afrika mashariki.. aaah wote wako sawa tu katika kuwajibika. Hata kama hawaombi rushwa, lakini kuzungusha na njoo kesho, njoo kesho :-( wanakuchelewesha kupata RB tuuuu wakati wewe unataka kuishia hapo
Ikitokea ukaibiwa na mtu unamfahamu na kumuamini, wakati mwingine inashangaza na kukaa unacheka tu, he he heee
Mwenzenu yamenikuta baada ya kukutana na mtu aliye na fani ya kuwa mwizi au mdokozi . Kijana aliyekuwa anaaminika kwa uaminifu na ushamba, ukimpa pesa kanunue kitu, anakurudishia mpaka senti tano. Ukimtuma kitu cha 5000 aka-bargain kwa 3000 anakurudishia chenji yote
Ukisahau coin kwenye mfuko anakuletea. Kwa miaka 8 hajawahi kubadili tabia.
Nimeachiwa kijana huyu miezi 10 iliyopita kwa sifa tele, na kweli alidhihirisha kuwa ni mtu safi kwa muda wote.
Lakini sijui kwa nini roho yangu ilikuwa inasita kufungua pazia la uaminifu wote kwa muda niliokuwa naye, na hivi karibuni niliamua kuwa muangalifu zaidi.
Lakini wapi bwana, jumanne wiki hii nikiwa kazini na nimefunga milango yote ya nje, ila ya ndani niliacha bila kufunga na funguo, na yeye akiwa kwenye servant qtr yake huko nje, kwa nini asinilize pesa zote nilizoacha chumbani, cha ajabu kakomba pesa za kitanzania, faranga za Rwanda na kuacha dola na shilingi za Kenya wakati zilikuwa pamoja!!
Kinacho niacha hoi zaidi, nusu ya faranga zote zilizokombwa zilikuwa sehemu ya mshahara wake!! ambao alikuwa hajachukua kwa maombi yake mwenyewe.
Mwisho wa siku, nimegundua sehemu alipopitia, kama huna ujuzi wa kuangalia hakika usingeweza kutambua, yaonekana hiyo kazi aliifanya kwa muda mrefu, na taratibu. Aliweza kutengeneza njia yake ambayo anaweza kuingia na kutokea ndani kisha kutoka nje tena, hakika sikudokezi ni wapi, maana mwingine anaweza kusoma hapa akaja akakuliza na wewe.....
Kwa ufupi, kijana mwenyewe hajulikani alipo kwa sasa...
Nimejifunza kufanya ukaguzi wa mara kwa mara.
Kinachoniudhi sasa! Kupata namba ya shauri. Ma- arufonsi wa huku hawajali time, sasa siku ya 3 eti bado niende kesho. Halafu kitu kidogo huku wala hawana habari kabisa. Hata kondoo wengine wakiambiwa subiri hapo wanakaaa masaaa yoote, mie nilikuwa sitoki mbali na mlango mpaka inabidi wanisikilize alaaaaaaaa!
I wish a lovely weekend. Usiseme pole, toa onyo ndugu weee, ili nikomae zaidi au vp?
8 comments:
Hahahahahaha..........
thanks for the BIG smile :-)
:)
Have a wonderful weekend
:))
Pole mkubwa! Nilitaka nikukope. Sasa dah!
Pole kwa yaliyokukumba, ila asante kwa funzo. Hapa nimejifunza mawili kwa haraka, Kuwa makini na kutokuamini 100% kila mara na Utaratibu wa kushughulikiwa na vyombo vya usalama nchini Rwanda pale raia anapokuwa na tatizo.
Sasa, mwizi aliingiaje? (najua umesema husemi, nimeisoma hiyo sentensi, lakini nimeamua kuuliza, kwani ulisema 'usiniulize?').
Pole kaka! na asnte kwa funzo.
hongera. lazima na wewe uliwahi fanya hivyo sehemu
KAKA HUJAMPATA TU MWIZI WAKO?
Pole kwa tukio hilo la maudhi. Nina imani mwney uwezo wa yote atakujalia heri na kupata zaidi ya hicho kilichopotea
Umesema tusiseme pole. Ila nasikitika kwa wiki nzima browser yangu ilikuwa ikikataa kufungua blog yako. Leo ndo nimeweza. Ahsante kwa funzo.
Uwe na wakati maridhawa.
Post a Comment