Member of EVRS

Wednesday 5 May 2010

Kenya yasamehewa na Dubai!

Serikali ya Muungano wa Falme za Himarati (United Arab Emirates) umeondoa kizuizi kwa wakenya kwenda Dubai kwa sharti kuu la kuwa ni lazima wawe na angalau shahada moja.
Kizuizi hiki kiliwanyima wakenya wengi fursa ya kufanya biashara kati ya Kenya na Dubai hasa kwa wafanyabiashara wadogo na wa kati ambao huwa ni wengi.


Mzozo huu ulikuja kutokana na makosa ya maofisa wa uhamiaji wa Kenya kuwatimua watalii kutoka Dubai kwa tuhuma kwamba ni magaidi. Kati ya waliotimuliwa ni pamoja na watu wa jamii ya Kifalme ya Himarati.

Viongozi wa kiserikali wa Kenya walihaha sana hadi kufikia muafaka, kwani ilikuwa inahatarisha ajira za wakenya wengi walioajiriwa Dubai ikiwa ni pamoja na shirika la ndege la Falme hizo la EMIRATES ambalo limeajiri maelfu ya wafanyakazi amabao ni wakenya kuliko idadi ya wafanyakazi wote wa shirika la Kenya Airways.

Serikali ya Kenya ilikuwa na haki ya kuwajibika kutokana na uzembe na uamuzi mbovu wa maafisa wake.

2 comments:

Subi Nukta said...

Hawa jirani zetu tukiwafuatilia vizuri ni somo zuri sana kwetu. Tujifunze kwa mazuri na mabaya yao ili tuweze kujenga kwetu vizuri.
Maamuzi ya kukurupuka mara nyingi hayafai!
Nimefurahi kuona Himarati wanawahurumia Wananchi ambao wangeteseka kwa maamuzi ya viongozi/watendaji wachache wenye dhamana.

EDNA said...

Heee hii ni kali.