Member of EVRS

Thursday 29 December 2011

Kiwango cha Elimu Jijini London, Uingereza Kinatia Aibu!

Nchi ya Uingereza ambayo inajivunia kuwa nchi mojawapo yenye ushawishi mkubwa katika masuala ya siasa na uchumi. Na pia kuwa taifa mojawapo duniani ambalo watu wengi hupenda kukimbilia huko wakitarajia kupata mavuno makubwa ya fedha kwenye mifuko yao. Na pia watu wengine kukimbilia kusoma huko wakiwa na imani ya kuwa vyeti watakavyovipata huko vitawasaidia kupata kazi kwa urahisi kwenye nchi zilizoendelea za Ulaya na Amerika. 
  
Hali hii inaweza kutoweka hivi karibuni ikiwa juhudi za ziada hazitafanyika kufanya marekebisho makubwa katika mfumo wa utoaji elimu nchini humo. 
  
Takwimu zilizotolewa mwezi wa Juni 2011, zinaonyesha ya kuwa asilimia 25 ya watoto wanaomaliza elimu ya msingi katika jiji la London hawajui kusoma wala kuandika, na wale wanaoenda sekondari, asilimia 20 ya hao wakimaliza elimu hiyo, pia hawawezi kusoma wala kuandika vizuri, na hata ukiwapa kitabu kusoma hadharani, hawajiamini kabisa. 
Habari hii haishii kwa watoto wa shule tu, bali hata watu wazima wanaofanya kazi jijini London, zaidi ya asilimia 15 yao, nao pia suala la kusoma na kuandika linawapa taabu sana! 
 
Habari hizi zilifichuka pale waziri mkuu wa sasa alipokuwa anasisitiza kazi zitolewe kwa vijana wa kiingereza badala ya wahamiaji. Wakati makampuni yatakayoendesha mashindano ya Olimpiki hapo mwakani yalipotoa nafasi za kazi na kuwataka vijana wa kiingereza kujitokeza na kujaza fomu za maelezo, vijana wengi wenyeji walikimbia na kugomea kujaza fomu hizo, ambapo waandaaji wa michuano hiyo walishangazwa na tukio hili. 
    
Katika mahojiano ili kufahamu kwa nini vijana wa kiingereza hawajitokezi, ndipo ilipobainika ya kuwa elimu ndio ilikuwa mgogoro, kwani vijana walikiri ya kuwa hawawezi kujaza fomu hizo kwa sababu hawajui kusoma wala kuandika!  
  
Hata hivyo, kuna mashirika mengine yamekuwa hayaajiri baadhi ya waingereza kwa sababu ama barua zao za maombi ya kazi zinakuwa na makosa mengi sana ya maneno (Poor spelling) ambapo ni karibu ya asilimia 40 za barua hizo hutupwa bila kuwaita kwenye usaili, au wanaoitwa, hudhihirisha wazi kuwa uwezo wao wa kusoma ni mdogo sana. Hii ilianishwa na habari hii hapa 
  
Kwa sasa mke wa Prince Charles,Camilla Windsor, anajihusisha na juhudi za kuongeza kutoa elimu bora kwa watoto wa uingereza ili baadaye waje kuendesha uchumi wa nchi yao ambao kwa sasa unaenda mrama kwani viwanda vingi vinakufa kwa uongozi mbovu, na kwa sasa uingereza uchumi wake unaendeshwa kwa kutegemea kukusanya kodi kwa wafanyakazi na wafanyabiashara ambao wengi wao ni raia kutoka nje ya Uingereza. 
  
Soma makala hii kwa kiingereza inayozungumzia elimu ya Uingereza kwa sasa

3 comments:

Anya said...

We want to wish you Chib and yours
A HAPPY & HEALTHY New YEAR
enjoy New Years Eve with your family

Hugs from your Dutch friends :)

DIGITAL WORLD PAGES ARCHIVE said...

Hello! Happy New Year! I wish all the bests to You in 2012!

chib said...

Thank you Guys. I wish you the same.
Welcome again next year!