Member of EVRS

Monday 19 December 2011

Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-Il Amefariki Dunia


Kim Jong Il


Rais Wa Jamhuri ya Korea (Korea ya Kaskazini) ama kiongozi mpendwa Kim Jong-il pichani hapo juu leo ametangazwa rasmi ya kuwa alikwishafariki dunia. 
Msemaji wa Serikali ya Korea Kaskazini, amedai rais wao mpendwa alifariki siku mbili zilizopita, yaani siku ya jumamosi tarehe 17 Disemba 2011. Inadaiwa ya kuwa alifariki kwa kupata mshtuko mkubwa wa moyo akiwa kwenye treni katika ziara ya ukaguzi, japo haujafafanuliwa ulikuwa ni ukaguzi wa nini. 
  
Vyanzo zaidi vya habari vinadai kuwa kilichochangia kifo chake ni uchovu mkubwa wa mwili na akili alivyokuwa navyo kiongozi huyu maarufu ambaye anakadiriwa alikuwa na miaka 69, japo mwaka aliozaliwa bado hauna uhakika sana kama ni kati ya mwaka 1941 au 1942. Ingawa anajulikana alizaliwa tarehe 16 February nchini Urusi, na alipewa jina la Yuri Irsenovic Kim kabla halijabadilishwa baadaye aliporejea Korea akiwa na miaka takribani 3.

Kim Jong-Un

Mtoto wake wa kiume ambaye ndio mdogo kuliko wote, Kim Jong -Un, mwenye umri wa miaka 27 ndio anatarajiwa kushika madaraka ya baba yake, japo umri wake bado ni kitendawili kwa madaraka anayotarajia kushikishwa. Kwa sasa mtoto huyu ndiye aliyechaguliwa kuwa kiongozi wa shughuli za mazishi ya Baba yake akiongoza jopo la watu 232 wanaoratibu mazishi hayo yatakayofanyika tarehe 28 Disemba 2011 jijini Pyongyang. 
   
Tangu Korea ya Kaskazini ikombolewe tarehe 15 Agosti 1945 imewahi kutawaliwa na viongozi wawili tu ambao no Kim Il-Sung na mwanaye ambaye amefariki sasa Kim Jong-Il ambaye aliingia madarakani kuanzia tarehe 8 Julai 1994 hadi kufariki kwake hapo tarehe 17 Mwezi huu. 
   
Kim Jong-Il alikuwa anatuhumiwa kuwa alikuwa ni dikteta kwa wananchi wake, na inadaiwa alikuwa hataki propaganda ya aina yoyote, hasa kutoka mataifa ya magharibi kuingia nchini kwake. Na inadaiwa vyombo vya habari nchini Korea ya Kaskazini vilikuwa haviruhusiwi kutangaza habari zozote za nje ya nchi yao!  Kimsingi vyote karibu vyote vya habari nchini Korea ya Kaskazini viinamilikiwa na serikali.
  
Pia kiongozi huyu alikuwa ni tishio kwa nchi majirani hasa kutokana kuwa na mpango wa kutengeneza silaha za kinyuklia kwa nia ya kuwatishia maadui zake ambao walikuwa ni Korea ya Kusini, Japan na Marekani. Hii inaweza kuwa ni moja ya sababu zilizofanya Korea ya Kusini kutangaza hali ya tahadhari mara tu ilipopata taarifa za kifo cha Kim Jong-Il.  

4 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Pole wanaKorea kwa msiba!!

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Nakipenda kifo kwa sababu hakichagui na kamwe hakiangalii makunyanzi. Safi sana !!!

RIP "Dear Leader"...Hakuna wa kukuhukumu isipokuwa YEYE; na asante kwa kusimama kidete dhidi ya mabeberu wa magharibi!
======>

Dakta:

Nilikuwa napita hapa kusema kwamba sasa nimerudi tena rasmi. Tupo pamoja !!!

http://matondo.blogspot.com/2011/12/wanablogu-wenzangu-na-wapenzi-wote-wa.html

chib said...

Prof Matondo, karibu sana

DIGITAL WORLD PAGES ARCHIVE said...

In several years we will see what will change...