Member of EVRS

Thursday, 15 December 2011

Wanafunzi Wasiojiweza Rwanda Kuendelea Kusaidiwa Ada ya Elimu

Mkurugenzi wa MTN Rwanda Khaled Mikkawi akikabidhi hundi ya msaada wa MTN-Rwanda kwa mlezi wa Imbuto Foundation Mama Jeannette Kagame
Mfuko wa Maendeleo kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu wa Rwanda (Imbuto Foundation) ambao mlezi wake ni mke wa Rais Kagame, Mama Jeannette Kagame, umepokea kiasi cha faranga za Rwanda Milioni 90 kutoka kwa kampuni ya mtandao wa simu ya MTN-Rwanda kwa ajili ya kuwasaidia vijana waliopo shule za upili kiwango cha kidato cha kwanza hadi cha sita kwenye masuala ya ada na gharama nyingine za shule. 
 
Mfuko huu ni mahsusi kuwasaidia watoto walio katika matatizo ya kimaisha ambao wazazi wao hawajiwezi au hawapo tena duniani. 
  
Tangu kuanzishwa kwake mwaka 2002, umeshasaidia zaidi ya vijana 5,000

Habari kutoka newtimes