Member of EVRS

Monday 8 August 2011

Vurugu Za Tottenham: Wa Kulaumiwa ni Nani?


Photo and English news from BBC
Watu wanaweza kujiuliza kwa nini mnamo kipindi cha mwisho wa wiki kulitokea Vurugu kaskazini mwa jiji la London katika eneo la Tottenham. 
  
Chanzo kikubwa ilikuwa ni mauaji ya mkazi mmoja wa eneo hilo ambayo yalifanywa na polisi tangu alhamisi ya wiki iliyopita. Inasemekana watu waliokuwa wanafuatilia sababu za kifo hicho katika kituo cha polisi hawakupata majibu ya aina yoyote au ya kuridhisha. Hivyo, waliamua kufanya maandamano ya amani kukizunguka kituo hicho.  
Wakaazi wa eneo hilo wanasema.. kwenye msafara wa mamba na kenge hawakosi. Maanadamano yaliyotarajiwa kuwa ya amani, yaligeuka kuwa ya vurugu, pale watu wachache waliaamua kuvamia maduka mbalimbali na kubomoa kisha kupora mali mbalimbali na kukimbia nazo.  
  
Baadhi ya mashuhuda walisema walikuwa wnawaona watu wakikimbia na seti za runinga, radio, vyombo vya elektroniki, blanketi, vyakula tena wengine wakitumia matoroli ya maduka waliyopora, na hakukuwa na hata askari wala gari la doria katika sehemu hiyo, na kwa hiyo wanaishutumu polisi kuwa iliachia kwa makusudi watu waendelee na vurugu hiyo.  
Lakini hakuna anayezungumzia polisi zaidi ya 30 waliojeruhiwa katika vurugu hizo!
   
Hata hivyo polisi wamepinga vikali ya kuwa waliachia waandamanaji waendelee na fujo! 
  
Kwa ujumla eneo hilo la Tottenham, ni maarufu kwa wahamiaji wanaotoka sehemu mbalimbali duniani hususan Afrika, na ambao wameshapewa uraia wa Uingereza, na wengi wao ni maskini, ambao wanaishi kwa msaada wa posho za kutokuwa na kazi, na wengine walikuwa wanafaidi posho zaidi kwa kuzaa watoto kwa wingi, kiasi kwamba ilifikia wakati walikuwa wanapata posho karibu sawa au zaidi ya wafanyakazi wa kawaida. Kwa kawaida posho hizi zimekuwa zikiongezeka kila mkaazi anapopata mtoto mwingine, japo serikali ya sasa imeanza kuzipunguza posho hizo ukizingatia ya kuwa "watu wasiotaka kufanya kazi" wamekuwa wakiongezeka. Punguzo hili hakika linawakera wakazi hao waliokuwa hawapendi kufanya kazi. 
  

2 comments:

gm, uk said...

sasa vurugu zimehamia maeneo mengine ya london, na bamingham, kundi la vijana wakiwemo wa chini ya miaka 18, wamevamia maduka hasa ya viwalo vya vijana na electroniki na kufanya shopping ya bure,mtoto umleavyo ndivyo akuwavyo, kuona kuwa hawatumii akili wamechoma na post office ambamo kila mwisho wa wiki huenda kuchukua mafao ya posho zao. polisi wanashindwa kwadhibiti ipasavyo maana hawana nguvu ya kimadaraka, haki za binadamu zinawabana nk,

Jumaa said...

Naona kuna dalili za ukichaa, sijui kama nimekosea.