Member of EVRS

Tuesday, 17 May 2011

Babu wa Loliondo Keshavuna karibu Shilingi Bilioni 2

Kutokana na hesabu zinazowekwa na watumishi wa Babu wa Loliondo, watu au wagonjwa zaidi ya milioni tatu wamekwishapata kikombe cha dawa tangu alipoanza shughuli hiyo mwezi wa august mwaka jana. 
  
Gharama kwa kila mtu ni ndogo, yaani shilingi mia tano tu, ambazo kwa utaratibu wa kawaida wa TRA haziwezi kuandikiwa risiti, kwani ni chini ya kiwango cha shilingi za kitanzania 1,000 ambazo kisheria lazima uandike risiti. 
 
Kwa hesabu za haraka, Babu Ambilikile amekwisha ingiza zaidi ya shilingi za kitanzania bilioni 1.5, na inakadiliwa akimaliza mwaka atakuwa amezidisha shilingi bilioni 2. 
 
Na kwa kipindi hiki, wataalamu wa hesabu, wanakadiria zaidi ya shilingi trilioni moja, zimekwishatumiwa na watu mbalimbali kwa ajili ya kusafiri kutoka sehemu mbalimbali duniani kuelekea Samunge pekee, ambapo Mchungaji Ambilikile yupo. Hii haijumuishi chakula, malazi, matengenezo ya magari na gharama nyingine zikiwapo za kupata vibali na mawasiliano. 
  
Hizi pesa alizojipatia mchungaji mstaafu hazina ufisadi, kwani kila mtu anajipeleka mwenyewe, japo mchungaji amesisitiza lazima akugawie yeye mwenyewe, sina hakika kama ni udhibiti wa mapato au kuepusha matapeli wasije ichakachua dawa yake. 
 
Lakini wezi wanaonywa, ya kuwa pesa hazikai Loliondo, na ukiziiba, basi vikombe vyote walivyokunywa watu vinajaa tumboni mwa mwizi.... 
 
Habari ndiyo hiyo.....

6 comments:

Fadhy Mtanga said...

ha ha haaaaa....kwamba pesa haikai Loliondo, lakini ukiiba vikombe vyote walivyokunywa watu vitajaa tumboni mwako. Sasa jamani zipo wapi huko?

Kaka Chib, sasa babu anazifaidi vipi pesa zake? Mie nadhani angesitisha huduma walau kwa mwezi moja akaenda zake Alabama, Hawaii, ama Bangkok akala zake 'guditaimu' kisha akarudi kuendeleza libeneke.

Rachel Siwa said...

kwikwiwkikwi nami nimefurahi kuwa eti mwizi akiiba vikombe vyote walivyokunywa watu vitajaa tumboni!!!Ngoja nami niongezee vikijaa tumboni mwa mwizi ndiyo atapona magonjwa yote na si ndiyo ataishi mileleeee au?

Simon Kitururu said...

Hili nalo ni neno!

Angestukia dili ya kikombe wakati yuko kijana angetanua kweli ,...
... kwa maana nasikia utuuzima unaleta vipingamizi katika matanuzi kwa kuwa kubwa zima kuna mambo mengine huwezi kuyafanya kwa kuhofia kuonekana limbukeni au una mambo ya kitoto!

CCM Oyeee!

Samahani nilitaka kusema Kikombe oyeee!

emu-three said...

Ndipo unapoona umuhimu wa `kutangaza biashara' sijui kama atakuwa na fadhila za kuwakumbuka `vyombo vya habari'...kwasababu kazi walioifanya sio mchezo...!

EDNA said...

Duuuh babu noma.

chib said...

Ha haa Kitururu, ulikuwa na nafasi ya kufuta hilo neno CCM kabla kuandika ati ulitaka kusema....