Member of EVRS

Tuesday, 10 May 2011

Kumbe! Kuna Tofauti ya Kiingereza cha Kuzungumza na Kuandika!

Kimya kikuu ..... 
  
Nilikuwa nyumbani kwa mapumziko mafupi, cha zaidi niliususia mtandao wa aina yoyote, ila , sikuachana na kupiga mitaa, hata nilipofika katikati ya Jiji la Darisalama, kwenye mtaa wa Mosque, nikakumbana na tangazo la kuwahabarisha wateja wa duka fulani ya kuwa kuna bidhaa mpya zilizoingia, tena bango lenyewe lilikuwa kubwaaa! 
  
Basi nilipata burudani tosha baada ya kuungua na joto na foleni zisizo na mwenyewe! 
 
Napenda kuwasalimu tena, baada ya kubisha hodi..

2 comments:

Swahili na Waswahili said...

Karibu tena kaka,Babu hajakupa zawadi yangu?.

Goodman Manyanya Phiri said...

Kosa kubwa kwa wasomi wa eneo hilo; wangemsaidia mfanyabiashara kuandikia lugha sanifu.


Anapoanguka ndugu yako usifurahie kamwe; kwani nawe hapo alipoangukia UMEANGUAKA hivyohivyo!