Member of EVRS

Tuesday 24 May 2011

Waasisi wa CCJ: Je, Tuwape Hongera?

Nilikuwa nafuatilia malumbano au sijui niiteje yanayohusu kuanzishwa kwa Chama Cha Jamii (CCJ) Ambayo kwa mtazamo wangu, ninaona kama yalikuwa yanalenga kuumbuana kwa baadhi ya wanansiasa.

Pia niliweza kumsikiliza kada mmoja wa CCM mwenye asili ya Arusha kupitia kwenye runinga akithibitisha kufanya mazungumzo na viongozi waandamizi walipo serikalini na kwenye Chama Tawala, ya kuwa ni kweli aliombwa na viongozi hao agombee ubunge kupitia CCJ mara usajili wake utakapo kamilika.

Wanao onekana kurusha "bomu" hili, wanaeleza madhumuni ya mpango wa kuanzishwa CCJ yalikuwa ni kupambana na ufisadi ambao ulionekana kukielemea chama tawala, na kama vile chama hicho kilikuwa kimefumba macho na kuziba masikio kukwepa sauti ya chura aliyekuwa anapiga kelele za kuwazomea mafisadi.  
Vyama vingine kama CHADEMA, NCCR-Mageuzi, CUF nk, navyo vipo katika mapambano makali dhidi ya mafisadi.  
 
Kwa mtazamo wangu.... mimi ninaona madhumuni ya CCJ yalikuwa mazuri katika kupambana na rushwa, wizi wa mali za uma, utapeli na kujilimbikizia mali kwa baadhi ya watanzania wachache ambao ni walafi na wasio na utu hata chembe kwa watanzania wenzao.  
Kwa maana hiyo, viongozi au mtu yeyote aliyekuwa mstari wa mbele kuanzisha CCJ ni mtu safi na anayekubalika, kwa mantiki hiyo, wanaotjwa kuwa ndio ufunguo wa CCJ wanapaswa kupongezwa. 
   
Nafikiri watu wengi watakubalinana nami, kwamba hii si kashfa, hawa watu walikuwa wanaona mbali, na inaweza kuwa ndio iliyokuwa changamoto, kwa chama tawala kuja na sera ya kujivua gamba, na chagizo kubwa likiwa limetokana matokea ambayo hayakuwa yametarajiwa na chama fulani, huku wale waliokuwa wanaona kwa macho, walishajuwa nini kitatokea.  
  
Tunaomba wenye "mabomu" ya aina hii, waendelee kuyaleta ili tuchambue mchele na pumba vizuri.

1 comment:

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

taarifa za kiintelijensia zinaonyesha kabisa kuwa nawwewe ni kati ya waanzilishi na ndio maana chama kilipotea kusikojulikana