Member of EVRS

Thursday, 12 May 2011

Mla Nyama za watu Aumbuka!

Katika mambo ambayo si ya kistaarabu, kuna mtu mmoja huko nchini Slovakia, aliingia kwenye mtandao wa internet na kuweka tangazo la kutafuta mtu aliyekuwa tayari kujiua na kukubali mwili wake uliwe na huyu jamaa chizi au asiye na ustaarabu.

Cha kushangaza, raia mmoja wa Uswisi alijitokeza na kuwa tayari kuliwa nyama pindi atakapomaliza kujiua. Lakini inaonekana Malaika Israeli alikuwa bado ana shughuli nyingi kiasi cha kushindwa kuja kuitoa roho ya Mswisi huyu.... kwani Mswisi huyo alibadili uamuzi wa kujiua, na hivyo kulifikisha suala lake kwenye vyombo vya usalama.

Baada ya hapo, polisi waliandaa mtego wa kumshika "mla nyama za watu", huku wakimtumia mtu aliyetarajiwa kuliwa kama chambo cha kumnasa huyo "mla watu".

Katika harakati za kumkamata huyo "mla watu", polisi mmoja alijeruhiwa baada ya kufyatuliwa risasi na mtuhumiwa, ingawa polisi nao walifanikiwa kumjeruhi vibaya "mla watu" huyo a.k.a mamba.

Angalia video na habari ya huyu chizi hapa

4 comments:

SIMON KITURURU said...

Binadamu kiumbe cha ajabu sana!

Yasinta Ngonyani said...

Haswaaaa binadamu ni kiumbe cha ajabu sana....

Anonymous said...

HEEEEEE!!!!!

Goodman Manyanya Phiri said...

"...huyu jamaa chizi au asiye na ustaarabu..."


Hapo nilikuwa na nakuu; lakini wote binadamu duniani chizi tuu. Tunatofautian tu kiwango cha ugonjwa wetu.


Kama ni ustaarabu, "ustaarabu" ni kitu gani wakati Wahindi wanamuona ng'ombe kama rafiki yao na hawali nasi huku tunakula? Mbwa tunamuona kama rafiki wa binadamu na hatuli lakini nasikia wenzetu Uchina ni nyama tamu.


Mimi naona tunacheleweshwa bure tu: kama jamaa anataka kumla binadamu kwa makubaliano, amle tu! DEMOKRASIA!!!