Member of EVRS

Monday 19 July 2010

Vuvuzela Zaendelea Kuwa Maarufu

Kwa wale waliokuwa wanazichukia vuvuzela za Afrika Kusini itabidi wabadili mtazamo wao... Kwani inaelekea zinaweza kutumika kama alama ya upenzi wa mpira wa miguu au timu ya mpira wa miguu.


Ujerumani ambayo ilikuwa maarufu kupitia pweza wake waliyempachika jina la Paul, inaendelea kuwa maarufu zaidi bada ya kampuni moja huko kutaka kutengenezewa vuvuzela kwa makadirio ya awali waweke oda ya vuvuzela milioni 5 (5,000,000). Kwa sasa bado wapo kwenye mchakato mkubwa wa kuweza kubuni vuvuzela ambayo itakubalika kwenye soko lao.


Inapenda kufanya mabadiliko kidogo kutokana na vuvuzela za Afrika kusini, kwani inadaiwa zile za Sauzi, zimetengenezwa kwa plastic hafifu (cheap plastic), na wao hawawezi kuzipata hizo. Pia za kwao wanataka ziwe na uwezo wa kutokuharibu mazingira (environmental friendly).


Pia inapenda vuvuzela zao ziwe na rangi 3 kama ilivo bendera ya nchi yao, yaani nyeusi, manjano na nyekundu, na pia iwe nyepesi zaidi ambayo itapunguza gharama za usafiri.


Kwa kuzingatia malalamiko ya wanachi wa Ujerumani, ya kuwa walipokuwa wanaangalia runinga wakati wa kombe la dunia, vuvuzela zilikuwa zinavuma kama vile jamii fulani ya nyuki... kampuni hiyo inataka kubuni vuvuzela ambayo itakuwa na kipunguza sauti (Silencer) ili isiwe kero kwa mashabiki watakaokuwa karibu na hiyo vuvuzela.


Wataalamu wa vuvuzela wa Sauzi wamekuwa wakisisitiza kuwa vuvuzela nzuri ni ile kubwa, lakini wajua ukubwa wa vuvuzela, maana yake sauti yake nayo inakuwa kubwa, nafikiri ndio maana hao jamaa wanataka kipunguza sauti....


Namkumbuka rafiki yangu Fadhy amabye ana matumaini makubwa sana kwamba vuvuzela zitakuja kuwa maarufu sana, hasa kwenye Ligi Kuu ya Uingereza.

3 comments:

John Mwaipopo said...

walipokuwa wanajaribu kuikataa vuvuzela shida haikuwa vuvuzela. shida ilikuwa ni ubunifu wa ki-afrika zaidi. wazungu hutamani kila kitu kizuri kianzie kwao. waafrika wakati huu wamedhihirisha kuwa wanaweza kuwa chanzo cha mambo mema kupitia vuvuzela.

o'Wambura Ng'wanambiti! said...

mmmmh!

Anonymous said...

Have [B][URL=http://www.fitnessworkoutclub.com/insanity-workout-dvds.html]insanity workout[/URL][/B] been aspiring to possess a six-packed abs lengthy sufficient or the sexy and tempting human body contour yet haven't obtained an inch [B][URL=http://www.fitnessworkoutclub.com]does p90x work[/URL][/B] closer to this most coveted dream? Be troubled no much more due to the fact the best muscle creating work out will assist and facilitate you to definitely materialize your personal fairytale ending- that 1 day you'll wake up biding your sweet goodbyes to your hated waist line and body fats. Your physique could have good effects if you possess a excellent constructing muscle work out . Even so, [B]does p90x work[/B] ought to be certain to combine and compliment the exercising [B][URL=http://www.fitnessworkoutclub.com]p90x reviews[/URL][/B] with the motivation and the desire to produce your build far better. In existence, building muscle mass without exercising is certainly not a wise and healthful concept. In spite of how busy you are, [B][URL=http://www.fitnessworkoutclub.com]p90x[/URL][/B] should always discover time to offer and give a break yourself with worthwhile actions which will allow you to make your human body fit and wholesome.

[URL=http://www.fitnessworkoutclub.com][IMG]http://www.beachbody.com/images/en_US/products/programs/insanity/ins_sell_chrisb_b.jpg[/IMG][/URL]