Member of EVRS

Friday 9 July 2010

Octopus Paul: Pweza Maarufu Kuliko Wote Duniani

Pweza (pichani juu) ambaye anatunzwa kwenye nyumba maalumu ya viumbe maji (aquarium) huko Oberhausen, Ujerumani amejizolea umaarufu mkubwa kwa watu wa Ujerumani na kwingineko duniani mara baada ya kufanikiwa kubashiri matokeo ya timu ya Ujerumani kwenye kombe la dunia huko Afrika Kusini kwa kupatia kwa asilimia 100 ya matokeo yote ya Ujerumani.


Habari iliharibika pale alipobashiri kuwa Hispania itashinda dhidi ya Ujerumani, kwa mara ya kwanza aliwakasirisha wapenzi wa soka wa Ujerumani kwani hawakufurahia kushindwa kuingia fainali ya kombe la dunia. Na ni kweli usiku huo Ujertumani ilifungwa na Hispania.


Kwa sasa kuna washabii walikuwa wanataka huyo pweza achinjwe na wamle kabisa. Kwani hakutarajia awaangushe. Lakini wao si wa kwanza kudai achinjwe na kuliwa, walioanza ni wale wa Argentina, pale alipobashiri kushindwa kwa Argentina na kweli wakafungwa mabao mengi tu.


Kwa sasa washabiki wa Hispania wanaomba huyo pweza apewe ulinzi wa kutosha ili asiuwawe, kiasi kwamba na Kiongozia wa Hispania amemtumia Kansela wa Ujerumani, Angela Merkert kuongeza ulinzi kwa Pweza huyo ambaye amebatizwa jina la Pweza Paulo (Octopus Paul).


Leo anangojewa kutoa utabiri wa fainali kati ya Hispania na Uholanzi.


Sijui itakuwaje akitabili Uholanzi kushinda, wahispania nao wataomba achinjwe? Ikumbukwe kuwa wahispania wanapenda saaaaaaaaaana nyama ya pweza.

Kuna washabiki wanaomba atunzwe mpaka kombe la dunia la 2014!
Wamiliki wa pweza huyo wameshasema watamtunza kabisa


Yangu ni masikio na macho tuuuu.


Photo from Telegraph.co.uk

4 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Nauungana nawe kaka Chib yangu pia masikio na mcho!!

Fadhy Mtanga said...

mie pia ningefurahi kupata nafasi ya kumla pweza huyo ili niwe na uwezo wa kutabiri mambo.

chib said...

Kaka Fadhy!!!! Hapo ni sawa na kuukata mti unaotoa matunda mengi na matamu ili uangalie huko ndani unafananaje!!

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

wewe, yaani mnafikiria kula wenzenu tu. heri ya mavegeterian woote wasiokula wanyama