Member of EVRS

Tuesday, 17 April 2012

Upotoshaji wa Habari za Tanzania

Jana nilikuwa ninasoma jarida la matangazo ya bidhaa za duka kubwa la vitu mchanganyiko (Supermarket) ambalo lilikuwa limenakshiwa kwa picha za kuvutia za bidhaa mbalimbali ambazo ninauzwa katika duka hilo.  
Mbali ya yote hayo, liliongeza baadhi ya habari za nchi za Afrika ya Mashariki ambazo zilijumuisha vivutio mbalimbali vinavyopatikana katika nchi za Afrika Mashariki. 
 
Niliposoma kichwa cha habari kinachohusu Tanzania... nilivutiwa ili nisome makal hiyo.
Kulikuwa na habari nzuri za vivutio kama mlima Kilimanjaro, ziwa Tnaganyika (Lake Tanganyika) na umaarufu wake, pia na bonde la Ngorongoro ambalo ni la kipekee Duniani lilipambwa vizuri.  
 
Tatizo...... 

Nilipoingia kwenye habari za lugha... nilishangaa wakidai ya kuwa lugha ya kigogo ndiyo inayoongewa sana Tanzania ikifuatiwa na kihaya, halafu kiha, tena kimakonde, na wakadai kiswahili hakimo katika lugha zinazo ongewa kwa wingi!!!! 
  
Nilipofika kwenye hoteli na mighahawa maarufu sana ya Tanzania, nilihisi siijui Tanzania....

Nikaona bora niishie hapo na kunywa maji ya baridi, sijui kupoza nini, lakini nilipata nafuu na kuendelea na kazi nyingine. 
 
Kwa anayejua habari sahihi za mambo hayo hapo juu, basi na anifahamishe ili nami niende na wakati!!

2 comments:

Anonymous said...

tumbaf kabisa.

emuthree said...

Itakuwa sasa ni kuandika tu, ilimradi kuna kuandika,ilimradi shabaha yako itimie....lakini je?