Member of EVRS

Wednesday, 11 April 2012

Hofu ya Kutokea Tsunami Yaondolewa


Tetemeko kubwa la ardhi lililotokea leo katika pwani iliyo karibu na Kisiwa cha Sumatra nchini Indonesia ambalo lilikuwa na kipimo cha 8.6 halikuweza kuleta Tsunami kama ilivyobashiriwa hapo awali. 
  
Mawimbi makubwa sana yalikadiriwa kuwa na ukubwa usiozidi meta 1 kutoka usawa wa bahari, na kuna sehemu nyingi walipata mawimbi madogo zaidi na hivyo hayakuleta madhara yoyote zaidi ya usumbufu kwa watu kukimbia na kuingiwa na wasiwasi. 
  
Kufuatia onyo hilo, shughuli nyingi za kwenye bahari ya Hindi zilisitishwa ikiwamo na nchi za ukanda wa pwani ya Afrika Mashariki ambapo ilikadiriwa pwani hii ingeweza kupigwa na mawimbi ya Tsunami hiyo kwenye muda wa kati ya saa 11 jioni hadi saa 2 usiku. 
  
Kutokana na habari zilizotolewa na kituo cha kutoa tahadhari ya Tsunami, ni kwamba Tsunami hiyo haipo tena, na wala watu hawana haja ya kuwa na wasiwasi.

No comments: