Member of EVRS

Monday, 23 April 2012

CCM Tunawaimarisha kuja kuwa Wapinzani Madhubuti Kwenye Serikali Ijayo - Mbilinyi

Mbunge wa Mbeya Mjini, mh. Mbilinyi amewapa somo wabunge wa CCM ya kuwa wabunge wa CHADEMA kuwapigia kelele wabunge na Serikali ya CCM ni kuwajenga kuwa wapinzani imara mara pale CHADEMA itakaposhikilia dola kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2015. Kwani CHADEMA haitataka kuwa na wapinzani legelege, inahitaji watu wanaoisimamia serikali iliyopo madarakani kwa ushupavu ili wao CHADEMA na serikali yao waende kwenye mstari ulionyooka.


 
Mh. Mbilinyi alikuwa anachangia muswada uliowasilishwa na kamati teule iliyochunguza tukio la kutoroshwa kwa wanayama hai mwaka jana unaohusisha wizara ya Maliasili na Utalii.

  
Taarifa hiyo imejaa kila aina ya takataka utakayoifikiria kutokana na yaliyojiri katika uchunguzi huo.

  
Baadhi ya matatizo yaliyoainishwa ni pamoja na
  • Waziri wa Maliasili na Utalii kujiamulia kutoa vibali kwa makampuni ambayo hayakuomba kibali cha uwindaji
  • Waziri kutoa vibali kwa makampuni ambayo hayakuwa na sifa japo kamati ya ushauri ilimweleza waziri kuwa makampuni hayo hayana sifa
  • Wanyama kusafirishwa wakiwa hai kwenda nje ya nchi bila maombi yoyote kutoka huko nje
  • Raia wa kigeni kupewa kibali cha kukamata wanyama wakati hivyo vibali hutolewa kwa watanzania tu
  • Baadhi ya viongozi wa chama ….. kuingilia shughuli za uhamiaji na kuwapitisha wageni wa shughuli za uwindaji kinyume cha sheria
  • Wanyama kufugwa/kuhifadhiwa kwenye makazi ya watu kwa zaidi ya hata miaka 8 wakati sheria hairuhusu wanyama kukaa sehemu kama hizo au kutunzwa kwa zaidi ya miezi mitatu
  • Vibali vya kukamata wanyama kutolewa kiholela na kwa watu ambao kisheria hawaruhusiwi kuto
  • Vitalu kutolewa bila kufuata sheria zilizopo za uwindaji
  • Kampuni iliyopewa kibali cha kusafirisha wanyama hai ya Jungle International haikuwa imeomba kibali cha kusafirisha wanyama, na pia kimsingi kampuni hiyo ilishabadilishwa jina na kazi miaka mingi na wakati inapewa kibali hicho haikuwapo kwenye daftari la msajiri, kwa maana nyingine ni kampuni hewa.   
Mambo ni mengi na kama una uzalendo na nchi yako unaweza kuivunjilia mbali radio unayosikiliza au runinga unayoitazama.

 

1 comment:

Upepo Mwanana said...

Usije ukanifanya niivunjilie mbali laptop yangu kwa kusoma ujumbe huu :-((