Member of EVRS

Thursday 19 January 2012

Rwanda Yapunguza Kodi ya Nishati ya Mafuta Kupunguza Makali ya Mfumuko wa Bei

Wakati mfumuko wa bei unaelekea kupanda hapa Rwanda, na hivyo kuelekea kupandisha bei za bidhaa mbalimbali za vyakula na matumizi mengine. Serikali ya Rwanda imeamua kupunguza tozo ya kodi kwa mafuta kwa asilimia 6% . Taarifa hii ya punguzo ilitolewa na wazara ya Biashara na Viwanda.
 
Hali hii imesababisha kushuka mara moja kwa bei ya mafuta kutoka Faranga za Rwanda 1,000 kwa lita moja ya mafuta ya petroli na dizeli hadi Faranga 940. Hii ni sawa na punguzo la asilimia 6% kwa kila lita inayonunuliwa.  Bei elekezi ilitolewa na wizara hiyo ikitegemea bei ya mafuta ya rejareja haitazidi Faranga za Rwanda 940 kwa lita.
 
Baada ya kutangazwa bei hii mpya, vituo vyote vilishusha bei na hakukuwa na tatizo lolote la vituo kuacha kuuza mafuta kama inavyokuwa Kenya na Tanzania. 
 
Hii ndio serikali inayojali mustakabali na uchumi wa wananchi wake.

2 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Haya...

emuthree said...

Aheri wenzetu wana kaubinadamu, hapa ndio wanapandisha ile kukomoa,halafu mbaya zaidi umeme wenyewe hakuna. Mimi naishi sehemu ambayo tunapata umeme kwa kupitia njia au mkondo, sijui wanaita grid, kitu ya Kisarawe, Huko bwana sasa hivi kilaikitinga saa moja, au saa mbili umeme unakatwa,kurudishwa ni majaliwa, au ndio mtindo ule wa kukata umeme na kuwasha, utafikiri kuna wanafunzi wapo kwenye masomo, wanafundishwa jinsi ya kuwasaha na kuzima....aibu tupu! Eti miaka 50 ya uhuru!