Member of EVRS

Friday, 17 June 2011

Siku 100 za Maombolezo ya Mauaji ya Kimbari, Rwanda


Wiki ijayo tarehe 4 Julai, nchi ya Rwanda itahitimisha kumbukumbu ya mauaji ya kimbari dhidi ya Watutsi yaliyofanyika miaka 17 iliyopita.
Ni siku muhimu kitaifa kwani wale wahanga wa vurugu hizi hukumbukwa kila mwaka kuanzia mwezi Aprili ambapo mauaji yalianza rasmi mara baada ya ndege iliyokuwwa imewabeba marais wa Rwanda na Burundi kupigwa na inachosemekana ni kombora la kivita muda mchache kabla ya ndege kutua kwenye uwanja wa kimataifa wa ndege, Kigali.
Kwa kipindi hiki cha kuwakumbuka wahanga hawa, watu mbalimbali hutembelea makumbusho ya wahanga hawa yaliyopo katika eneo la Gisozi jijini Kigali ambapo kuna makabuli ya jumla, kumbukumbu za mifupa na mafuvu ya baadhi ya watu waliouawa, picha na taarifa mbalimbali zikiwepo video za matukio hayo.

Wiki hii, ofisi yetu nayo ilikwenda kuzuru eneo hili la kumbukumbu ya mauaji, zaidi ya wafanyakazi 100 tulikondoka mchana kazini kwetu, ambapo ilibidi wabakie watumishi kwa ajili ya huduma za dharura, na wengi wetu tulijumuika kwenda kupata historia ya mauaji hayo na pia kutoa mchango utakaowawezesha waliosalimika kwa heri na kwa ubaya ili waweze kuendelea kupata huduma ambazo kwa ajili ya ama ulemavu walioupata, au kuambukizwa virusi vya ukimwi kwa makusudi na wauaji ambavyo vimewafanya kushindwa kumudu maisha ya kawaida.
Ni historia ambayo kwa kweli inatia huzuni sana, na wakati mwingine unashindwa kuelewa kwa nini watu waligeuka na kuwa zaidi ya wanyama.

Na picha ya mwisho hapo ni ishara ya mwenge wa matumaini na amani, ukiashiria wamedhamiria kutokurudia tena balaa kama hili.

Kwa wale watakaofika Kigali, hii ni sehemu ya kutembelea kwa kujifunza.

3 comments:

Herrad said...

Hi Chib,
Thanks for sharing this moving and informative post.,
Please call by my blog and pick up your awards.
I hope you enjoy passing them on as I have.
Its good to visit you and read your posts.
Love,
Herrad

emu-three said...

Ni tukio la historia na kama watu hawatajifunza kwa tukio hilo..basi tena, lakini bado wapo hawajifunzi, mapigano, chuki na tamaa za uongozi bado zinatuandama.....!

Rachel Siwa said...

Mungu awabariki na kuwapa moyo wa kusamehe,lakini kweli yamekwisha?nina rafiki yangu ikifika siku hiyo wanakutana pamoja na ndugu zake kula,kulala pamoja pia wanakuwa na hasira sana mpaka namuogopa.Nao walipoteza baba na dada katika tukio hilo.

Ahsante kaka Chib kwa kutukumbusha.