Member of EVRS

Tuesday, 14 June 2011

Bunge la 10 ni Vioja Mbele kwa Mbele

Kila mara ninapokaa na kuangalia moja kwa moja kupitia kwenye runinga majadiliano ya miswada kweny Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.... Huwa naishia kucheka.
Si kwa kuwa naona linajadili mambo ya manufaa kwa nchi yetu pekee, na kutoa michango yenye tija, bali huwa nashuhudia vituko vya wabunge na kejeli wanazozitoa, wakati mwingine bila hata kujali ya kuwa wapo ndani ya Bunge ambalo ndilo limewapa jina la kuitwa "waheshimiwa".

Bado nafikiri dhana aliyokuwa nayo muasisi wa Taifa letu, Mwalimu Nyerere, ya kufuta wabunge kuitwa waheshimiwa, na badala yake waitwe "ndugu" ilikuwa na maana, na maana yake inaonekana kwa sasa ndani ya Bunge.

Jana jioni kulikuwa na zogo la kama kwenye kilabu cha pombe za kienyeji wakati wa michango ya hotuba iliyotolewa na ofisi ya rais - mahusiano na sera. Kwani kuna wabunge waliwashutumu baadhi ya wabunge wenzao ya kuwa ni waombaji rushwa, wengine walisema kuna vyama fulani kila siku ni maandamano tuu, wengine walikuwa wanasema kuwa kuna wabunge ni mabingwa wa "domo kaya" ambalo lilisababibishwa wafukuzwe kwenye vyama vingine kabla ya kujiunga na vyama walivyomo sasa nk.

Mwendelezo wa majadiliano ulikuwa unakatizwa mara kwa mara kwa taarifa na anagalizo.
Baadhi ya Wabunge ambao ni waheshimiwa walikuwa wanachombeza maneno wakati wengine wakiwa wanaongea. Nahisi mwenyekiti wa kikao hicho cha jioni alikuwa na wakati mgumu 
 
Kuna saa niliona napoteza muda kuwasikiliza hawa waheshimiwa... 
 
Mwanzo Spika alisema wabunge wengi ni wapya, yaani ni takribani asilimia 70, hivyo bado hawajajua vizuri kanuni za bunge, lakini ... sina hakika lini watazijua kanuni hizo na kuwa waheshimiwa wa kweli, kwani tangu wameteuliwa kuwa wabunge wamekwisha gonga miezi karibu minane, na kama mpaka leo hawajui kanuni... basi ni mabutu kweli.....

Nahisi hii sera ya kuongeza viti vya wabunge ilikosewa, nahisi tunahitaji wabunge wachache lakini walio makini....... Just thinking aloud!

Image from loadtr

6 comments:

emu-three said...

Wapya kwa manthari, au sio, lakini sio kiutendaji, kwani miezi imeshakatika, twataka kazi...tumewatuma nini jamani, maisha magumu, nchi giza, foleni kila mahala...mkumbuke cheo ni dhamana!

Swahili na Waswahili said...

Mungu ibariki Tanzani!

SIMON KITURURU said...

Babu wa Loliondo eeeh! Kwa hili la kutibu BUNGE letu tukufu nalo huwezi kusafiri ili kutibu hili?:-(

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

hata blog hii kuna wakati huwa bunge na hivyo huwa kioja pia

Faustine said...

...Heri mimi sijasema.....

chib said...

@ Faustine, ha ha haaa