Member of EVRS

Friday, 20 March 2009

Jadi zetu


Ukisema Mbegeeeee, watu wanaitika wachaggaaaaaaa. Ila wachagga wenyewe wanitika leta hapaaaaaaa.
Naam, ndio hao hapo juu. Kuna wakati nilitembelea sehemu za Uru kwa mwaliko, nilivutiwa na watu hawa kwa kuona wamefanya mabadiliko kidogo katika unywaji wa mbege, badala ya kutumia chubuku moja kwa wote, hapa kila mtu alikuwa na ya kwake, hii ni hatua nzuri kwa kuepuka viini tete vya kudhuru afya ambavyo vinaweza kusambaa kwa kutumia chubuku moja kwa wote. Kilichonivutia zaidi ni heshima wanayopewa watu wakubwa, yaani watoto kupewa mbege kabla ya wakubwa, hapana!
Nilichokuwa najiuliza, ni kuhusu vazi la kofia kwa wanaume, sijui pia ni tamaduni au fasheni, maana karibu wote walifika na kofia.

No comments: