Member of EVRS

Monday, 21 November 2011

Thursday, 17 November 2011

Mchakato wa Muswada wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba Mpya ya Tanzania

Nimenukuu:
Maoni ya Dk. Faustine Ndugulile (Mbunge wa Kigamboni) kuhusu mchakato na muswada wa sheria ya mabadiliko ya Katiba mpya

Nchi yetu inatimiza miaka tarehe 9.12.2011. Kwa hiyo mjadala wa kufanya mapitio ya katiba yetu umekuja muda muafaka kwa taifa hili. Ni muda mrefu umepita na hivyo ni jambo jema kutafakari tulipotoka kama Taifa, tulipo na tuendako.

Tumekuwa na katiba ya mwaka 1977 ambayo imekuwa ikutuongoza hadi hivi sasa, lakini kama taifa tumeamua kuanza mchakato utakaopelekea kuwepo na katiba mpya itakayodumu vizazi na vizazi vijavyo.

Nashukuru kuwa sehemu ya mchakato wa kupitia muswada wa sheria ya mabadiliko ya katiba ambayo itaongoza mchakato mzima wa kupata katiba mpya.

Kwa babati mbaya sana muswada huu umezua mjadala mkubwa ndani na nje ya Bunge. Baadhi ya wananchi, wanaharakati na wanasiasa wanataka muswada huu usijadiliwe kutokana na sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kupinga uwasilishwaji kwa mara ya pili, wananchi kutopata fursa ya kuchangia na mamlaka ya Rais kwenye mchakato huu.

Ninaungana na watanzania wote wanaotaka katiba mpya. Ninaungana na watanzania wote wanaotaka katiba nzuri na yenye kuweka maslahi yaTaifa mbele na yenye kulinda haki za msingi za Raia wa nchi.

Sasa hizi tofauti zinatoka wapi? Kwanini kumekuwa na mtazamo tofauti katika suala hili?

Jioni ya leo nimejaribu kuwasiliana na watu mbali mbali kupata mawazo na maoni yao kuhusu muswada huu unaoendelea kwa sasa. Nimegundua yafuatayo:
  1. Baadhi ya watu hawana ufahamu mzuri wa kitu gani kinachoendelea kwa sasa. Baadhi ya watu wanafikiri kuwa ndio tumeshaanza kuandika hiyo katiba mpya pasipo kuwashirikisha wananchi.
  2. Uelewa wa nini kilicho ndani ya muswada bado ni mdogo hata kwa wale wasomi.
Vilevile kuna matatizo mengine. Kuna watu ambao kipato chao cha kuendesha maisha kinatokana na mchakato huu wa Katiba Mpya. Watu hawa wanapata fedha nyingi za wafadhili na baadhi yao wanaleta mkanganyiko wa makusudi ili waendelee kushibisha matumbo yao. Wapo wengine wanaouangalia mchakato huu kwa mtazamo wa kiitikadi, kidini, Uzanzibari na Utanzania Bara. Ukichanganya yote hapo juu na upotoshaji unaendelea kwenye mitandao na vyombo vya habari, unakuta suala hili linazidi kuwachanganya wananchi.

Kimsingi kinachofanyika sasa hivi ni kutengeneza sheria itakayoweka utaratibu wa kuandaa katiba mpya. Binafsi nimeisoma mara kadhaa na ninaona inakidhi mahitaji iliyokusidiwa. Nasema hivyo kwa sababu zifuatazo:
  1. Maboresho yanayozingatia hoja zilizotolewa na wadau wengi zimeongezwa kwenye muswada huu. 
  2. Nchi ya Zanzibar ambayo ni wadau wa Muungano wamepata uwakilishi wa kutosha. Raisi wa Tanzania Bara na Raisi wa Zanzibar watashirikiana katika kila hatua ya mchakato wa katiba hii. Hakuna atakayefanya maamuzi ya peke yake.
  3. Madaraka ya Rais yanayolalamikiwa yamepunguzwa sana kwenye muswada huu. Kwanza, Maraisi wote watashirikiana kutoa maamuzi. Pili, hadidu za rejea zimeshainishwa badala ya Raisi kuja na za kwake. Tatu, sifa na vigezo vya wajumbe wa tume zimeshainishwa.Kwa hiyo majukumu ya Raisi ni machache sana na maamuzi mengi yatafanywa na wananchi.
  4. Ushirikishwaji wa wananchi utakuwa ni mkubwa. Nchi nyingine zimeweza kutengeneza katiba kwa kupitia Bunge la Katiba au chakato wa kura za maoni (Referendum). Sisi Tanzania tumeamua kutumia njia zote mbili. Wananchi watashirikishwa kwa kutoa maoni yao kwenye mikutano ya tume inayosimamia mchakato wa katiba mpya, wananchi watashirikishwa kwenye mabaraza ya mapitio ya katiba, wananchi watashirikishwa kwenye Bunge la Katiba, wananchi watashirikishwa kwenye kura za maoni (Referendum).
Kwa mtazamo wangu ni vyema tukakamilisha muswada huu ili kazi kubwa na ya msingi iliyo mbele yetu iweze kuanza. Kuna mambo ya msingi ambayo kama Taifa tungependa kujadili ikiwa ni pamoja na mambo yafuatayo:
  1. Muundo wa Serikali-Tungependa Serikali iwe kubwa kiasi na ya aina gani, masuala ya Serikali ya Mseto (ikiwa chama kinaongoza uchaguzi kikashindwa kupata zaidi ya nusu ya kura zote), mamlaka na madaraka ya Raisi, uthibitishaji wa Bunge kwa viongozi n.k.
  2. Usimamizi na uthibiti wa Rasilmali zetu kama vile ardhi, madini, gesi na kama tutabahatika kupata mafuta. 
  3. Mfumo wa Bunge tunalotaka
  4. Uwakilishi wa wananchi wasio na vyama (Zaidi ya watanzania millioni 30 si wanachama wa vyama vya siasa) na suala la wagombea binafsi 
  5. Masuala ya uwakilishi wa jinsia na makundi maalumu kwenye sehemu za maamuzi
Tutumie muda mwingi katika hatua zinazofuata ili kujadili mambo ya msingi kama nilivyoainisha baadhi yake hapo juu.

Mchakato wa katiba ni mrefu. Niwasihi watanzania wenzangu tujadili kuhusu katiba tunayotaka pasipo kuweka masuala ya udini, maslahi binafsi, itikadi na sehemu ya Jamhuri tunapotoka. Tufanye hivi pasipo kuweka jazba na fujo. Tukifanya hivi tutafika salama. Wanaharakati watumie fursa hii kuwaelimisha wananchi haki zao na pia kuwapa elimu ya kutosha ili waweze kuchangia kwenye mjadala huu. Wanaharakati wasitumie fursa hii kufanya fujo, kuleta vurugu na kupotosha umma.

Mimi binafsi ningependa kuona tunapata katiba yenye maslahi kwa Taifa letu na vizazi vitakavyokuja baadaye. Tuna deni hilo kwao. Hatma ya Taifa hili iko mikononi mwetu. Hekima na busara zinahitajika sana wakati huu. Tutangulize Utaifa kwanza na maslahi ya nchi hii mbele.

Mungu Ibariki Tanzania

Dk. Faustine Ndugulile-Mbunge Kigamboni

15/11/2011

Dr Faustine angependa kupata maoni yako katika suala hili ili kuweza kumjenga kihoja katika kutambua watanzania wanapenda nini katika suala hilo. Kwa mtizamo chanya au hasi.

Saturday, 12 November 2011

Short-cut to Heaven!

 Enjoying the siesta!

 Yesterday... was watching the game till dawn!!!
It doesn't cost a thin' here!!

Ha ha haaa

Friday, 11 November 2011

Dr. Hemed Abbas Kilima: Ninavyokukumbuka

Sekta ya Afya ya Tanzania imempoteza Mtaalamu aliyebobea katika fani ya macho, Dr Hemed Abbas Kilima (Pichani juu) aliyefariki jana tarehe 10 Nov 2011 kutokana na ajali mbaya ya gari.

Hayati Dr Kilima alikuwa anasafiri kutoka Mbeya kuelekea Dar es Salaam alipopata ajali hiyo pale gari aliyokuwamo ilipogongwa na basi eneo la Al-Jazeera.  
 
Ni habari ya masikitiko kwa wana-taaluma wa afya hususan upande wa macho.  
  
Dr Kilima, mpaka anapoteza uhai wake akiwa bado ni kijana wa miaka 42 tu, alishapata shahada tatu katika fani ya afya zikiwa ni pamoja na:-
  • Shahada ya udaktari wa binadamu kutoka chuo kikuu cha tiba za Afya na sayansi ya Jamii - Muhimbili
  • Shahada ya uzamili katika fani ya macho kutoka chuo kikuu cha Tumaini
  • Shahada ya afya ya jamii kwa macho kutoka London School of hygiene and tropical medicine

Mbali ya hayo, alikuwa ni
  • Daktari bingwa wa magonjwa ya macho kwa watoto (Fellow- Paediatric Ophthalmology) aliyojifunza CCBRT - Dar es Salaam.
  • Fellow wa Eastern Africa college of Ophthalmology
  • Mwenyekiti msaidizi wa chama cha madaktari na wanataaluma wa Macho Tanzania.  
  
Ninamkumbuka Dr Kilima, kwani kwenye kozi ya shahada ya uzamili kwenye fani ya macho (Master of Medicine - Ophthalmology), tulikuwa darasa moja na tulikuwa wawili tu, mimi na yeye, kwa hiyo tulipitia hatua nyingi kimasomo ikiwa ni pamoja na kusoma, kufanya kazi, kufanya tafiti na kujiandaa kwa mitihani. Mbali na hayo tulikuwa tunasafiri sehemu mbalimbali pamoja ndani na nje ya nchi katika kutekeleza majukumu ya fani yetu. 
  
Tulipeana ushauri wa mambo mengi katika masomo na kujiendeleza kitaaluma, na kama tulikuwa tunafuatana katika kisomo na kujiendeleza kama vile mmoja akibandua mguu mwenzie anafuata, na hata nilipomaliza fellowship yangu naye baadaye alijiunga na kozi kama hiyo kwa fani tofauti kidogo tu, na alihitimu vyema mwaka uliopita.  
  
Na pia ndie niliyemuachia mikoba ya Mwenyekiti msaidizi wa Chama cha madaktari na wanataaluma wa afya macho Tanzania kabla sijapata nafasi zaidi katika shirikisho la taaluma hii kwa Ukanda wa Afrika mashariki (Ophthalmological Society of Eastern Africa).  
 
Mpaka anatutoka, alikuwa ni Daktari anayefanya kazi katika hospitali ya rufaa ya Mbeya, na mratibu wa macho kwa kanda ya kusini na nyanda za juu. Hivyo, Taifa limempoteza mtu muhimu ambaye bado alikuwa na muda mrefu wa kuendeleza huduma ya afya na kuwainua wengine. 
 
Binafsi nimempoteza mwenza na mshirika mkubwa kikazi, na pia nimempoteza rafiki wa karibu ambaye nilitarajia kushirikiana naye sana kuweza kuinua fani ya afya ya macho kwa Tanzania. 
  
Bwana alitoa, bwana ametwaa. 
 
Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi, Amen.

Tuesday, 8 November 2011

Vote for Mount Kilimanjaro as one of The New 7 Wonders of the World



Mount Kilimanjaro is located in Northern Tanzania, it lies few degree below the equator line.
It is the highest mountain in African continent, the highest point is at Kibo peak which is 5,895 metres above sea level.
It is an amazing mountain because of its location along the tropic, and its peak is covered by snow through out the year. Everything is natural.  
 
Apart from that, the whole of its basement is occupied by wild animals living freely without causing harm to neighbouring villages. 
  
Visiting and climbing this mountain, you will not only reach the highest point in Africa, but also you will enjoy seing ecological diversity and fresh atmosphere which is almost the same all year round. 
  
Few kilometres from Mount Kilimanjaro, you will be able to see the second highest mountain in Tanzania, mount Meru located in Arusha, and if you move further to north west you may get an opportunity to visit Ngorongoro crater, which is one of great wonders of the world filled again with all diversity you may think in the tropics.  
 
Natural beauties of mount Kilimanjaro has attracted me to vote for this mountain to be among the new seven wonders of the world. What about you? Just follow this link and follow instruction to cast your vote for Mount Kilimanjaro by using telephone or online. 
In Tanzania, you can vote through SMS by sending a message to number 15771 from any telephone network.
Sala pekee hazitoshi, piga kura yako tafadhali!
  
The deadline for voting is on 11th Nov 2011 (11.11.11)

Friday, 4 November 2011

Man's Facial Image Seen in Ultrasound


A mystical image or sheer coincidence? Either way, that’s one sad ‘nad.
Doctors in Canada were scanning through ultrasound images of a 45-year-old man with a painful mass in his testicles when they did a doubletake. There was a man's face staring up at them, the mouth grimacing as if he were in agony.
"It looked like a man screaming in pain, which I thought was hilarious considering the clinical picture of the poor guy," Dr. G. Gregory Roberts, School of Medicine at Queen's University, Kingston, Ontario, told msnbc.com

Roberts and urologist Dr. Naji J. Touma reported their amazing discovery -- which ranks right up with the grilled cheese Madonna or pancake Jesus -- in a recent issue of the medical journal Urology.
In the article, "The Face of Testicular Pain: A Surprising Ultrasound Finding," the doctors revealed that, upon spotting the distinctive tumor, a "brief debate ensued on whether the image could have been a sign from a deity (perhaps "Min" the Egyptian god of male virility; however, the consensus deemed it a mere coincidental occurrence rather than a divine proclamation."

Click here for full article

Thursday, 3 November 2011

Tuesday, 1 November 2011

Joseph Machele: Mtanzania Aliyepata Nishani ya Heshima ya Franklin Nchini Mexico

Joseph with assistant of the Ambassador to the US Embassy in Mexico city  Mr.  John Feeley Deputy Chief of Mission.caption

Joseph na Mkewe Mariana

Rafiki na wafanyakazi wenzake Joseph - Ubalozi wa Marekani Mexico
Joseph Machele, Mtanzania ambaye anaishi Mexico city nchini Mexico, amepata tuzo ya heshima ya Franklin (Franklin Award) ambayo hutolewa kila mwaka kwa wananchi wa Marekani au wanaofanya kazi katika idara za serikali ya Marekani ambao mchango wao kwa Taifa la Marekani katika fani mbalimbali za kazi zao umepita kipimo na kuweza kusababisha ufanisi mkubwa wa kazi au kuleta faida kwa uchumi au hali ya usalama kwa Marekani. 

   
Joseph Machele ambaye ni Mtanzania anayefanya kazi katika ubalozi wa Marekani nchini Mexico, ameweza kupata tuzo hiyo kwa utumishi bora na kuwa mbunifu. Allipata siku ya tarehe 12 Oktoba 2011, baada ya kupewa na naibu balozi wa Marekani nchini Mexico Bw. John Feeley.
Kupitia kujituma kwake na maarifa yake binafsi, aliweza kuokoa zaidi ya dola za kimarekani 115,000 kwa mwaka mmoja ambazo zingetumika kulipia gharama za kusafirisha samani na vifaa vya kukodisha na vitu vingine vidogo vidogo kwa ajili ya makazi ya watumishi wageni wanaoenda kufanya kazi kwenye ubalozi wa Marekani nchini Mexico.  
 
Mbali ya Joseph Machele kupata tuzo ya heshima, pia alijipatia kitita cha dola kama zawadi yake katika juhudi zake binafsi akiwa kazini. Alifanikiwa kuokoa kiasi hicho cha fedha kwa kuwashawishi wanaokodisha vifaa hivyo kutoa usafiri wa bure kusafirisha vifaa hivyo, jambo ambalo maafisa wa ubalozi wa Marekani walikuwa wanadhani ni kitu kisichowezekana kabisa. 
  
Hongera sana mdogo wangu Joseph kwa juhudi zako binafsi. Nakufahamu sana tangu kwenye ujana wako, ni mtu ambaye upo makini sana katika kazi zako. Usiishie hapo tu, bali ongeza bidii zaidi kwani mafanikio yako ni sifa kubwa kwetu sote tunaoishi Bara pevu na lenye utajiri mkubwa.