Member of EVRS

Friday 30 March 2012

Airtel: Yazindua Huduma zake Rwanda

Kampuni ya huduma za mawasiliano kwa njia ya simu ya Airtel inayomilikiwa na Bharti ya India, leo imezindua huduma zake nchini Rwanda na hivyo kuongeza idadi ya nchi ambazo Airtel inatoa huduma zilizopo barani Afrika kufikia 17. 
  
Nchi ambazo kwa sasa zinafikiwa na huduma za Airtel katika bara la Afrika ni Burkina Faso, Niger, Nigeria, Zambia, Kenya, Tanzania, Uganda, Chad, Malawi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Congo Brazaville, Sierra Leone, Madagascar, Ushelisheli (Seychelles), Ghana na Gabon. 
  
Bharti Airtel Ltd, ina mpango wa kuwekeza kiasi cha dola za Kimarekani milioni 100 katika kipindi cha miaka 3 ijayo. Kati ya hizo, dola milioni 30 zitatumika katika kupata leseni ya uendeshaji!  
  
Pia, kampuni hii inatarajia kutoa zaidi ya ajira 300 kwa wananchi wa Rwanda, nyingine zikiwa ni za moja kwa moja na nyingine si za moja kwa moja.  
 
Inatarajiwa gharama za kutumia simu zitapungua kwa sababu nguvu ya ushindani kwa sasa itaongezeka baada ya makampuni yanayotoa huduma hizo kwa sasa kufikia matatu. Mengine ni TIGO na MTN. 

Sunday 25 March 2012

Monday 19 March 2012

Wednesday 14 March 2012

Jiolojia: Afrika kugawanyika na Kuwa Mabara Mawili!

Wanasayansi wa jeolojia ambao wamekuwa wanafanya utafiti wa namna bahari inavyotokea katikati ya nchi kavu hivi karibuni wamegundua mvutano mkubwa wa sumaku katika bonde la Afar nchini Ethiopia. 
 
Mvutano huu wa sumaku ndio unaosemekana kuwa chanzo cha mkondo wa bahari kutokea mahali. Na mara nyingi hufanya kuwa tofauti ya nguvu za kisumaku katika tabaka la udongo, hii ni kutokana na miamba moto kusogea juu karibu na uso wa ardhi na kisha kupoa. Inapotokea mvutano wa kisumaku kutokea, miamba hii huanza kutoa nguvu za kisumaku kuelekea upande mwingine kuliko ilivyokuwa awali na hivyo kukinzana na miamba ya awali, na hivyo kuchochea miamba kusigana na kuachanana hivyo kutengeneza mkondo mpya wa bahari. 
 
Mara nyingi mivutano kama hii huonekana kwenye maeneo ya bahari kuu. 
  
Iwapo msukumo huu wa kisumaku utaendelea, basi kuna uwezekano wa bara la Afrika kugawanyika katika sehemu mbili zikitengwa na bahari. 
  
Ili kuweza kuwa na ufa inakadiriwa kuwa itaweza kupita miaka kama milioni 2, na kuweza kuacha nafasi ya mkondo wa bahari, inakadiriwa itahitajika kama miaka milioni 2 mingine ipite.  
Kwa hiyo watakaoshuhudia bahari hiyo, ni wale watakaokuwa wanaishi duniani mika akam milioni 4 ijayo.
  
Mimi sina utaalamu wa aina yoyote ya jiolojia, Kama unayaamini haya, basi habari ndiyo hiyo, inapatikana hapa pia 

Sunday 4 March 2012

Chelsea: Yamtimua Kocha Wake Andre Villas-Boas

Klabu ya mpira wa miguu ya Chelsea ya jijini London, leo imemfutia kazi ya kuifunza timu hiyo kocha Andre Villas-Boas baada ya kutetereka katika michezo ya ligi kuu ya England na pia mashindano ya Ubingwa wa ulaya. 
  
Kufuatia kupoteza mechi ya jana dhidi ya timu ya West Bromwich Albion kwa bao 1 - 0 wakiwa ugenini kulihamasisha uamuzi wa uongozi wa Chelsea kumuondoa kocha huyo mwenye umri wa miaka 34.
 
Kupoteza mechi hiyo ya jana kuliweka rekodi ya Chelsea kushinda mechi 3 tu kati ya 12 za mwisho za ligi kuu ilizocheza. 
 
Andre amedumu kwa siku 257 tu ndani ya Chelsea tangu alipoanza kazi ya kuifundisha Chelsea kuanzia tarehe 22 Juni 2011. Katika kipindi chote alichokuwa Chelsea, kocha huyu amekuwa akidaiwa ya kuwa alikuwa na migongano na wachezaji "wazee" ndani ya Chelsea, lakini haijathibitishwa ya kuwa ndio chanzo cha Chelsea kufanya vibaya msimu huu.
 
Kwa muda wa siku 10 zijazo, Chelsea itakuwa na kazi kubwa ya kuishinda timu ya Napoli ya Italia katika mashindano ya klabu bingwa Ulaya baada ya kupoteza mechi ya awali nchini Italia kwa kufungwa magoli 3 - 1.
Kabla ya hapo watalazimika kucheza mechi ya ugenini dhidi ya timu ya Birmingham kwenye mashindano ya kushindania kutwaa Kombe la chama cha soka cha Uingereza (FA Cup). Itakumbukwa ya kuwa mechi ya kwanza iliyochezwa kwenye uwanja wa Stamford Bridge, timu hizo zilitoka sare ya bao 1 - 1 huku Chelsea ikitoka nyuma na kusawazisha bao hilo. Kwa sasa, timu ya Birmingham ndio mabingwa watetezi wa kombe hilo.