- Kusikia mafanikio yaliyopatikana kitaifa kutokana na mchango wa wafanyakazi katika kulisogeza mbele gurudumu la maendeleo.
- Kujua ni nani amekuwa mfanyakazi bora katika taasisi wanazozifanyia kazi ili kuwapa hamasa ya kufanya kazi zaidi ili na wao waje wapate tunuku hiyo kwa miaka inayokuja
- Kujua mipango ya serikali yao katika shughuli zijazo za maendeleo
- Kutaka kujua nyongeza ya mishahara itakuwa kiasi gani, na vilevile kujua itapunguza kivipi ukali na gharama za maisha yao ya kila siku.
Lakini kwa mwaka huu, matumaini na tashwishwi imebadilika sana kwani badala ya watu kungojea kwa hamu taarifa ambazo hapo awali ndizo zilizokuwa zikiwapa matumaini wafanyakazi, kwa sasa wanasubiri kudra za Mwenyezi Mungu ili awashushie baraka kimiujiza za kupunguza ukata.
Cha ziada kwa mwaka huu, wafanyakazi wamekaa mkao wa kusubiri kama kiongozi wa nchi yao atasema chochote kuhusiana na tuhuma nzito za uhujumu uchumi na wizi wa mali za uma unaowahusu wateule wake ambao wengi wao wamekosa dira, kujitambua, sifa za uongozi na uzalendo kwa nchi yao na kugeuka kuwa vichaka vya ubadhirifu, wizi na ubinafsi huku wakiendelea kujisafisha kwa kujipakaa madhambi yao kwenye miili yao na kuonekana kama ....
Ninavyofikiri kwa sasa, ni kwamba kunahitajika mabadiliko makubwa ya mfumo wa utawala, uongozi, na wateule waliopo na kupata utawala mbadala, ambao unaweza kuwafanya watanzania wapime na kuwalinganisha waliopo madarakani kwa sasa na wale watakaokuja. Baada ya hapo, nina imani wateule watawajibika kwa wanachi vyema kwani wananchi watakuwa wameshapima na kujiridhisha ya kuwa hawa wanatufaa, na hawa hawafai....
Huu ni mtazamo wa mtu binafsi. Ameutuma ujumbe huu na kuomba niuchape ili watu waupime na kumuunga mkono au kumkosoa.
Happy May Day!