Member of EVRS

Thursday, 20 October 2011

Habari Tata: Gadhafi Kakamatwa / Kauawa?

Kuna taarifa zisizo rasmi zinazodai ya kuwa aliyekuwa Kiongozi wa Libya kwa muda mrefu, Mwanamapinduzi Kanali mstaafu Moammar Gadhafi ameuawa baada ya kujeruhiwa miguu yote miwili katika shambulio la anga la NATO lililolenga msafara wa Gadhafi alipokuwa anatoroka mji wa Sirte.
Inadaiwa ya kuwa chanzo cha kifo cha Gadhafi ni majeraha aliyoyapata kwenye miguu yake. 
 
Kuna madai mengine yanayosema ya kuwa aliyekuwa kiongozi wa mashambulizi ya Majeshi tiifu kwa Gadhafi, Abu Bakr Younus Jabr naye ameuawa katika shambulio hilo.  
  
Wakati huo huo, wasemaji wa jeshi la waasi wa Libya, wanadai ya kuwa wamemkamata Gadhafi akiwa hai katika mji wa Sirte, na kuwa alikuwa amejificha katika shimo na aliomba asipigwe risasi! Kuna muasi mmoja anadai alishuhudia kukamatwa kwa Gadhafi.  
  
Hata hivyo, habari hizi bado alijathibitishwa na kujua ukweli upo wapi.

1 comment:

emu-three said...

Zipo hata picha zake zinazoonyesha alivyouliwa, ...sasa je amanii itarejea Libya, na je ndoto zao zitatimia, yetu macho!