Member of EVRS

Tuesday 18 January 2011

Tanzania Yageuka Shamba la Bibi

Sina mengi ya kusema... Lakini bado nipo kwenye mshangao kwa jinsi ninavyo ona Tanzania inavyochumwa na kila mtu mwenye nafasi yake tena kuchuma usichopanda, na kuwanyima wenye njaa ambao ndio mali yao.

Wakati bado tupo kwenye kelel za kwa nini Tanzania iilipe kampuni ya kitapeli ya Dowans mabilioni ya pesa ambayo serikali yetu tukutu iliamua kupunguza kwa kuwahadaa watanzania kuwa ni tubilioni tisini na badala ya mamia... Sasa kuna uzushi mwingine kuwa Tanzania inatakiwa kuwalipa .... hawa kampuni kutoka India iliyoingia ubia na serikali wa kuendesha reli ya kati kiasi cha shilingi bilioni 21 kwa kuvunja mkataba tata ambao kampuni ya India ilishindwa kabisa kuendesha reli ya kati.

Najua watu wakipiga kelele utasikia tunatakiwa kulipa bilioni 12 tu, kama vile hayo mabilioni ni vijisenti tu!!

Sijasikia hata mara moja hiyo inayojiita serikali kusema ni hatua gani itawachukulia walio sababisha hasara na kututaka tulipe mabilioni ya fidia kwa kutokuwa na huduma ya aina yoyote!!

Kwa sasa nimeanza kuwa na wasiwasi haya mabilioni hayalipwi kwa kampuni yoyote ya nje, bali yanaenda kwa watanzania hao hao ambao ni makuwadi wakubwa wa ufisadi, na ndio maana kuna kuwa kama kuna haraka vile ya kutaka kulipa kabla ya bunge kuanza.

Hivi tumefumba macho au tumekaangwa akili.
Hakika mganga huyu ni mkali sana, sasa tusemeje, maana tumelala na lazima tutafute visingizio kama vile kilichotokea ni bahati mbaya.  
  
Hata wezi wa EPA waliambiwa warudishe taratibu tu, hawatachukuliwa hatua, na hakuna anayejua ni kiasi gani kilisha rejeshwa iwapo ni kweli.  
  
Wale watuhumiwa wa ujambazi kama akina AM walishikwa na baadaye wakaachiwa kwa kuambiwa ati wasifanye matukio ya uhalifu kwa angalau miaka miwili.   
 
Vinara wa madawa ya kulevya, orodha iliandaliwa, mwendesha mashtaka akatamka kuwa orodha inatisha, kuna jamaa fulani alikabidhiwa naye kaimeza kimyaaa, sijui anasubiri wikileaks tena!!!!!   

Shule zetu, watoto wanakaa kwenye vigunia, hospitali hakuna dawa wala wataalamu, maji hakuna, umeme sina la kusema, maana kuna jamaa yangu alisema ati Tanesco ni kampuni pekee duniani iliyoweza kufanikisha kupandisha gharama za kuuza umeme kwa kuongeza muda wa kuwaweka watu gizani badala ya kuwapa umeme!!!  
     
Hivi hawa watanzania siku wakifumuka, patatosha????  
   
Shamba la Bibi linavunwa tuuu, hivi haliishi hilo?

3 comments:

Anya said...

I wish the best for Tanzania
I wish I could help !!!!

Simon Kitururu said...

Tanzaniaaaaaaaaaa!:-(

Lakini atadakwa mtu tu siku moja na wote waonao huu ni ujanja ndio kitawatokea puani.

Hivi ni watu waainagani wanaingia hii mikataba?

Upepo Mwanana said...

ipo siku tu!