Last week I visited Arusha town, after more than 3 years without stepping my feet to this beautiful city.
It was dusty, and after walking about, I noted my shoes were powdered by vumbi!
I visited one of the shoe shiners ( Jamani hii kazi imekodiwa na wachagga), while waiting for my shoes to be ready, alas! I was given makata mbuga to wait while protecting my socks from dust.
Makata Mbuga, are local sandals, famously know as "Arusha to Moshi" by people living in this area. They are made from rejected or old car tyres. Maasai version of makata mbuga are more interesting!
The city is beatiful and clean, at least to the areas I visited
Lakini.. when you go to Ngaramtoni, yaani ongeza sponji kwenye kiti, na chunga sana kichwa chako, kwani barabara ipo kwenye mashimo, na sio mashimo yapo kwenye baarabara.
Habari mpya nilikutana nayo njiani wakati Naelekea Namanga wakati wa asubuhi baada ya chai, kwani kuna baba mmoja wa kimasai, tulimkuta ana kijana mdogo wa kiume kama miaka 7 hivi kavalia sare za shule siku hiyo ya jumapili!!Tulisimama, akasema, ero sopai!, nami nikajibu sopai orubaiyan, akaomba....saidia napeleka mutoto panado, yeye anasuka kuni boma ya ... ole parkw..., na mutoto yeye najua kabsaa, .. eeeh , tukamalizia kwa ashee, ashee nale. Naye akawahi kurudi kwa sangiki yake.
Kusema ukweli, huyo baba anajua umuhimu wa elimu, wikendi mtoto anarudi nyumbani, jumapili anawahi tena asubuhi, kwani shule ipo kama km 12 kutoka kwenye boma ya huyo baba, na aliposhukia ni porini..., kama kilomita 2-3 kufika shuleni kwao (Longido mjini).
Mchana, nilikuwa Nairobi, baada ya lunch, nilichukua taksi, kwa jinsi dereva alivyokuwa anaongea, na mate yanaruka kupitia geti la chini(Mwanya wa kutengeneza kwa kung'oa meno ya chini), hakika ni mluo, akadai pale nilipomkuta haparuhusiwi madereva wa kabila jingine, na hasa wakamba, ati wakienda kupaki pale ni nuksi, na kuna mkuu wa polisi fulani anawakingia kifua kwa ukorofi huo. Kwa kuwa alikuwa peke yake, akawa na wasiwasi watakuja kupaki, hivyo alinikimbiza airport kama mbio za langalanga, I had to ask him if he has helmet!!!, kwani mkanda niliona hautoshi, nikihofia kupata head injury kama atakutana na hump, kwani naweza kurushwa kwenye roof, anyway niliwahi airport, kwani nilikuwa karibu kuchelewa!!!
Usiku, nilifika Kigali, dereva wa taksi aliingia mitini, ati alisikia baridi pale airport na ndege yetu ilichelewa kwa dk 45!!, bahati nilipata usafiri wa mabasi yanayopaki karibu kabisa na airport ambayo yalikuwa hayana watu wengi, kwani nilikuwa na kimkoba kidogo tu, na kulikuwa hakuna taksi. Nikamaliza safari yangu kwa kupanda mabasi mawili hadi kufika kiotani kwangu, na yote yakiwa na makonda wanawake/wasichana, wakihangaika kupiga debe kila kituo! Ila wenyeji walikuwa wanayakwepa kwa kuwa yana ongezeko na pesa zaidi kidogo kuliko yale ya kawaida.
Sheeee