Member of EVRS

Friday, 7 December 2012

Timu za Taifa za Tanzania Zimefungwa Nusu Fainali ya Cecafa Tusker Challenge cup 2012

Timu za Tanzania, Zanzibar Heroes na Kilimanjaro stars hazikufanikiwa kuingia fainali ya Cecafa Tusker Challenge cup mwaka huu wa 2012 baada ya kushindwa kwenye michezo yao ya nusu fainali. 
   
Timu ya Zanzibar imetolewa kwa maamuzi ya penati,, baada ya kumaliza kwa sare ya magoli 2 - 2 na timu ya Harambee stars ya Kenya. Zanzibar Heroes walikosa penati mbili za mwanzo.
 Mwisho ushindi ulisomeka kama hivi: Kenya 6 - 4 Zanzibar 
  
Nayo timu ya Tanzania Bara ilifungwa kwa jumla ya magoli 3 - 0 na timu ya Uganda, (the cranes) baada ya kuzidiwa maarifa ya mchezo.  
Timu ya Tanzania ilionekana kushindwa kwenda mbele, na badala yake mipira mingi walikuwa wanarudisha nyuma kuelekea golini kwao badala ya kushambulia mbele.  
  
Magoli ya pili na tatu yaliyofungwa na Uganda, yalitokana na uzembe wa walinzi wa Kilimanjaro stars kutokukaba kwa wakati wakidhani wachezaji wa Timu ya Uganda walikuwa wameotea.  
  
Kwa mantiki hii, Zanzibar na Tanzania bara zitakutana katika mchezo wao wa mwisho kutafuta mshindi wa tatu siku ya jumamosi tarehe 8 Disemba 2012.   Baadaye kwenye uwanja huo huo, Uganda itacheza na Kenya katika Fainali ya kutafuta bingwa wa mwaka 2012/13.

No comments: