Member of EVRS

Sunday, 18 November 2012

Kujivua Gamba na Kuliacha Likining'inia

Siasaaaa

Siasa kwa kweli ni mchezo wa kujaribu kuvutia na kufanikiwa kuteka fikra za wafuasi na watu wengine.
Pia siasa unaweza kuitafsiri kama ni dhana au mawazo aliyonayo mtu, na kujaribu kuwa aminisha watu wengine, ya kuwa hayo mawazo ya mwanasiasa huyo ni sahihi, na kama yakifutwa kwa makini, basi yatawasogeza watu kutoka sehemu moja kwenda nyingine yenye maendeleo zaidi. 
   
Wakati mwingine, mwanasiasa mwenyewe hana uhakika kama yupo sahihi, lakini anajaribu kuwavutia watu tu ili afanikishe malengo yake.  
  
Miezi kadhaa imepita tangu watu fulani waliposema walikuwa ni kama mfano wa wanyama wanaotambaa na wenye damu baridi, wakaueleza uma ya kuwa wamebadili safu yao na kuanza vita na mafisadi kwa mfumo wa kujivua makoti ya zamani na kubakia na makoti mapya. 
  
Lakini .... naona sina kumbukumbu kama walivua makoti au walinyofoa mifuniko ya makoti yao tu. 
  
Sasa tunasikia tena wamebadili safu na wamekuja na usemi ule ule wa vita tena ile ile..... 
  
Kwa hiyo tusubiri tena mwaka 2014 wakibadili safu za serikali za vijiji, tena tutasikia nini tena!! aaah  
  
Kwangu, nafikiri hakuna sababu ya kuendeea kuwapa nafasi watu wenye ahadi tuuuu au vipi!  
 
Ninachukia siasa za ahadi hewa!  Tubadilike alaaa!!

No comments: