Member of EVRS

Thursday, 24 January 2013

Hongera Joseph Machele kwa Kazi Nzuri Mexico!
Nakupa pongezi nyingi mdogo wangu Joseph Machele kwa kazi nzuri unayoifanya kwenye ubalozi wa Marekani nchini Mexico.

Hapo awali ulipata tuzo ya Franklin, kwa kazi nzuri na ubunifu wa hali ya juu mpaka ukapewa heshima ya kuitwa Guru na cheti.

Na sasa umepata tuzo nyingine. Nina imani hautavimba kichwa kwa kukijaza maji, bali utavimba kichwa ili upate nafasi zaidi kwenye ubongo wa kufikiri na kuongeza ufanisi katika kazi zako.

Hongera sana!!2 comments:

Joe Machele said...

Dr. Chibuga, asante kwa ushauri wa busara, hakika nitavimba kichwa ili nipate nafasi zaidi kwenye ubongo wa kufikiri na kuongeza ufanisi katika kazi yangu. We the people kama alivyosema mheshimiwa rais mteule wa marekani alipoapishwa.

Yasinta Ngonyani said...

Hongera sana!!