Member of EVRS

Monday, 15 November 2010

Wapinzani Wanaelekea Kuungana Bungeni

Kuna dalili ya kuwa wapinzani ndani ya Bunge la Tanzania wataungana mara pale Aliyekuwa kiongozi wa upinzani katika bunge lililopita Mhesh. Hamad Rashid Mohamed kutamka ya kuwa wapo tayari kushirikiana na vyama vyote vya upinzani kuunda umoja ndani ya bunge na hasa kwa kutoa mawaziri vivuli.  
  
Na pia alisema ya kuwa hawana nia ya kuwania uongozi katika kambi ya upinzani, bali kushirikiana kwa pamoja katika harakati za kukuza demokrasia ndani ya bunge na pia kuendelea kuikosoa Serikali kama walivyokuwa wanafanya katika bunge la 9. 
  
Mwanzoni, kulielekea kama kuna mfarakano ambao chanzo chake hakikujulikana, na watu walihisi zilikuwa ni zile kauli za Lipumba kujiona kuwa ni bora zaidi kufuikia hatua ya kujifananisha na mlima kilimanjaro, na kumfananisha mgombe aurai wa Chadema Mhesh Willbirod Slaa kama kichuguu.  
  
Tuna imani ya kuwa CCM nao wanalitambua hilo, na hivyo watakuwa makini sana katika shughuli za kuendesha mijadala na uwajibikaji ndani ya bunge, vinginevyo 2015 wataendelea kupoteza nguvu yao bungeni na mwisho kitakachofuata wanakijua.

6 comments:

John Mwaipopo said...

kwa siasa za nchi hii zilipofikia kwa sasa CUF si chama cha upinzani tena. upinzani wake una matege kwa kuwa tumeshaambiwa kwa upande wa zanzibar si CUF wala CCM walioshinda bali ni wazanzibar wote. tukumbuke CUF ina mashiko huko zanzibar ukilinganisha na bara ambako wana jimbo moja tu la Lindi mjini. Hii moja kwa moja inakwambia hoja ya CCM haipingwi na CUF na kinyume chake. kwa lugha ya picha CCM na CUF wanalala shuka moja.

kwa kutanabaisha haya nadhanai kama kimahesabu wanatosha, CHAMEMA waunde upinzani rasmi pasi na kushirikiana na vyama vingine. kimantiki tu CHADEMA ina wabunge makini kuliko vyama vingine. Hata katika uwanda wa hoja, CHADEMA wana historia ya kutoa hoja bungeni na nje ya bunge zilizoleta mvuvumko na changamoto katika taifa tofauti na hoja nyingi zilizotolea na wapinzani wengine ambazo nyingi zilikuwa chepechepe na zilizopauka.

Kama kuna ulazima wa kuungana basi ni heri wakaungana na NCCR-mageuzi (kungine washaitwa NCCR-Manunuzi kwa kununuliwa kisiasa ama kutokuwa na misimamo thabiti). NCCR-mageuzi huwa wana kigugumizi katika kutetema mambo ya msingi na mara kadhaa wamekuwa wakiunga mkono hata masuala yasiyofaaa kuungwa mkono.

TLP ndio kabisaa haina haja ya kusema sana. tumeshamuona na kumsikia mzee wa kiraracha akichumia tumbo. inawezekana kabisha yale aliyokuwa akiyasema kumsifia mwenyekiti wa CCM yana hoja na mashiko lakini kama hivyo ndivyo kwa nini na kwa sababu gani mtu kama huyu aitwe mpinzani ama aungane kutengeneza upinzani.

Bado naona CHADEMA si watoto yatima kisiasa. Wanaweza kutengeneza upinzani madhubuti pasi na kushirikiana na chama ambacho nusu ni tawala na nusu ni upinzani.

Fadhy Mtanga said...

...kama CUF ni mshirika wa serikali katika upande wa pili wa Muungano ambako ina nguvu zaidi, haidhuru kuiita chama tawala. kwa mantiki rahisi tu, chama tawala hakiwezi kuunga kambi ya upinzani bungeni. upinzani dhidi ya nani?

...kimahesabu, kinadharia, na kwa vitendo pia, chama mbadala cha upinzani hapa Tanzania ni CHADEMA. chama chenye wasomi na wajenzi wa hoja haswa. chama chenye kuleta changamoto. chama chenye mashiko ya wapenda mageuzi wote.

kwa idadi ya wabunge ilio nao, Chadema kinao uwezo wa kuwa na kambi ya upinzani yenye nguvu sana.

....hivyo vyama vingine kama kile cha jogoo, nilishapoteza imani navyo siku nyingi sana.

....wakati ndo huu...mchakamchaka umeanza.

Juma Maneno said...

Nakubaliana na waheshimiwa hapo juu. Hata kwenye nafasi ya unaibu spika, CUF wameshatangaza mtu. Naona kama CUF itapoteza uelekeo wa upinzani bungeni.
Nakubaliana na John, ya kuwa Mzee wa Kiraracha hana kitu zaidi ya CCM iliyovaa kofia ya TLP.
CHADEMA wajizatiti wao wenyewe, NCCR Mageuzi mnhu! Kwanza wanataka kufungua kesi ya uchaguzi wa Kawe ambapo CHADEMA imeshinda, wakidai ati TAMWA ilimpigia debe mwanachadema ashinde.

Yasinta Ngonyani said...

Ama kweli kazi ipo!!

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

sijui wanapinga nini

chib said...

Kamala... :-)