Member of EVRS

Friday, 5 November 2010

JK Mshindi wa Urais Tanzania kwa 61%

Tume ya Taifa ya Uchaguzi imemtangaza Jakaya Kikwete kuwa mshindi kwa kupata jumla ya alama 61.1% ya kura zote akifuatiwa na Slaa wa CHADEMA aliyepata 26.3% na wa tatu ni Lipumba ambaye safari hii kaporomoka na kupata 8%.  
  
Ushindi uliopungua wa JK haukutarajiwa na wana CCM wengi, kwani walikuwa wana imani atapata ushindi wa kimbunga wa zaidi ya 90%, lakini mambo yamebadilika kabisa.   Ikumbukwe kuwa uchaguzi wa 2005, JK alipata zaidi ya 87% ya kura zote  
   
Slaa hakuhudhuria kwenye ukumbi wa matokeo, lakini wagombea wengine wote walikuwapo.  
  
Wapiga kura Uchaguzi wa mwaka huu walikuwa 42.6% tu ya wale wote waliokuwa wamejiandikisha.

1 comment:

Upepo Mwanana said...

Nahisi CCM watakuwa wamepata funzo fulani, na itaweza kupunguza jeuri isiyo na maana kwa baadhi ya viongozi wake.