Member of EVRS

Wednesday, 24 November 2010

Naomba Ushauri

Sehemu ninayoishi hapa Kigali, ina usalama wa hali ya juu, na patrol za polisi usiku zipo karibu muda wote! 
   
Tarehe kama ya leo, yaani 24 Mei 2010, mfanyakazi wangu wa nyumbani (house boy) alirudi kutoka "kijijini" alipoenda kusalimia famlia yake, na aliporudi usiku nilishtukia tu yumo ndani ya ua, bila kufunguliwa geti.
Nilipomuuliza kaingia vipi, akasema alifungua mlango kwa ndani kupitia kidirisha cha ulinzi (Security window), kwa ujumla sikuamini amini. Siku iliyofuata niliporudi kutoka kazini nilikuta katoweka, baadaye niligundua upotevu wa fedha kutoka chumbani kwangu.  
Habari ilifikishwa polisi, na hakuna kilichofanyika.  
   
Kijana huyo alikuwa naaminiwa sana na kila mtu, lakini mimi tangu siku ya kwanza roho yangu ilimkataa. Japo familia yangu walielekea kumwamini na kumpenda. Sasa naona wamebadilika kuliko hata mimi!

Leo tarehe 24 Novemba( Sielewi kwa nini ni hii tarehe), miezi sita imetimia, wakati naingia gereji kujiandaa kuondoka kwenda kazini, niliona nyendo zisizo za kawaida kwenye kona ya gereji, nilipokaza macho zaidi nikaona macho ya blink hapo kwenye kona huku yakiwa yamefunikwa na mlango mbovu na viti chakavu. Nilipokamua macho zaidi, mara akaibuka kijana yule yule aliyekuwa mfanyakazi wangu. Akadai aliruka ukuta usiku kupata mahali pa kulala na kisha alikuwa anasubiri nikienda kazini, naye ajiondokee zake!  
   
Kwa sababu kwa sasa naishi mwenyewe, nilitoka nje kuomba msaada wa mlinzi ili nimdhibiti, lakini alifanikiwa kwa muda kuchomoka na kukimbia, lakini weeee, watu wanajua kupiga mitama ama ngwara, hakufika mbali ndo hivyo tena akaibusu ardhi.  
  
Baada ya kumfkisha polisi, akakiri alikwiba siku za nyuma. Na ni kweli aliruka ukuta kuingia ndani ya nyumba bila idhini yangu.  
HUWEZI AMINI ALIHUKUMIWA KIFUNGO HAPO HAPO, na kwa sasa amekwisha anza kutumikia kifungo jela.  
Hakuna kesi mahakamani wala kuhangaishana na kuleta ushahidi. kwani kila kitu kilikuwa hadharani.  
   
Upekuzi wangu pale alipokuwa amejificha, nilikuta sanamu ya plastiki ya mnyama mwenye pembe 2 ambazo zipo sharp. Hiyo sanamu nilishawahi kuiona ndani ya nyumba miezi mingi wakati naingia, nikaitupilia jalalani. Pia sanamu hiyo nilipoikuta, siku za nyuma nilishawahi kukuta sanamu ya mtu aliyevishwa hirizi ya mbao!  
   
Mimi ni mtu wa imani kidini na huwa sitetereki, kawaida yangu ni kuzichoma moto takataka kama hizo.  
  
Bado najiuliza, kama nikimwona tena baada ya kifungo ndani ya himaya yangu nimfanye nini.  

8 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Chib! kama ulivyosema wewe ni mtu wa imani kidini kwa kweli tupo wengi kwa hiyo hapa kazi ipo....

John Mwaipopo said...

huyo kijana hana nia njema na wewe asilan/abadan. amefungwa miaka mingapi? huyo hata akitoka huko rupango ungali ukiishi kwenye hiyo nyumba atakudhuru tu. mosi jaribu kufanyia marekebisho ya mfumo wa security wa nyumba (mageti, madirisha na milango). ikibidi install security system za umeme na zinginezo.

katu si mtu mwema huyo before prison na after prison.

hayo matakataka yake dawa yake ni moto tu.

emu-three said...

Wewe ni mtu imani, muombe mungu amsaidie huyo kijana, aione haki na aache tabia hiyo mbaya na akitoka awe mtu mwema!
Kwasababu wewe ni mtu wa imani usimfikirie vibaya, huenda katika kufikiria kwako kuwa atakuwa mtu mzuri, mungu atakubali dua yako ya wema na akabadilika!

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

duhu safi sana, walizi wako waliniambia kuwa usiku huo waliota unaingiliwa na kija huyo! sasa kama wewe ni mtu wa Imani, walinzi ni wa nini? kuna alindaye kufikia sirGod? au huombi sara za kiMungu?

ukija kumuona siku nyingine atakuwa anamalizia kipigo kitakacholeteleza mauti yako!

ushauri wangu ni kwamba wewe ukimwona mwachie achukue kile alichokifuata, baada ya hapo hatarudi tena!

ila imani yako ni haba na dnio maana unatumia walinzi wasinaziao na bigbro

chib said...

Ilikuwa ni kupata maoni tu, nashukuru kwa yote yaliyo wima na yaliyopinda.

Kamala umechemsha kaka, sijasema nina walinzi, nilisema nilienda kuita walinzi kutoka nje, maanake nje ya ya sehemu ninayoishi, kwani nisingeweza kumkabili na kupiga simu kwa mara moja. Kijana huyo ana shida moja, kila tukikutana uso kwa uso lazima ajikojolee au ..., sasa sioni sababu ya kumwogopa na mwoga wa namna hii!

Fadhy Mtanga said...

pole sana kaka Chib kwa yote...naamini ushauri uliopokewa utaufanyia uchambuzi...nakuombea kila la kheri

Jumaa said...

Huyo kijana anajidanganya tu. Mambo ya giza hayo kaibiwa na mganga. Alipofanikia kuiba alitumia uenyeji wake tu, si ajabu alikuwa na funguo za nyumba nzima

Upepo Mwanana said...

Kazi kubwa!! Watu wanapenda sana njia za mkato. Hata wakiambiwa kujipaka kinyesi ati hawataonwa, basi watajipakaa tu.
Ewe Mola pishia mbali haya matukio