Member of EVRS

Monday 30 April 2012

Mei Mosi Isiyo na Matumaini Wala Furaha

Hapo zamani za kale ....... Ilipokuwa inafika siku ya mei mosi, wafanyakazi walikuwa wanaingojea kwa hamu kubwa kwa sababu mbalimbali. Kwani siku hiyo walikuwa wanatarajia :
  1. Kusikia mafanikio yaliyopatikana kitaifa kutokana na mchango wa wafanyakazi katika kulisogeza mbele gurudumu la maendeleo. 
  2. Kujua ni nani amekuwa mfanyakazi bora katika taasisi wanazozifanyia kazi ili kuwapa hamasa ya kufanya kazi zaidi ili na wao waje wapate tunuku hiyo kwa miaka inayokuja
  3. Kujua mipango ya serikali yao katika shughuli zijazo za maendeleo
  4. Kutaka kujua nyongeza ya mishahara itakuwa kiasi gani, na vilevile kujua itapunguza kivipi ukali na gharama za maisha yao ya kila siku.  
  
Lakini kwa mwaka huu, matumaini na tashwishwi imebadilika sana kwani badala ya watu kungojea kwa hamu taarifa ambazo hapo awali ndizo zilizokuwa zikiwapa matumaini wafanyakazi, kwa sasa wanasubiri kudra za Mwenyezi Mungu ili awashushie baraka kimiujiza za kupunguza ukata.  
Cha ziada kwa mwaka huu, wafanyakazi wamekaa mkao wa kusubiri kama kiongozi wa nchi yao atasema chochote kuhusiana na tuhuma nzito za uhujumu uchumi na wizi wa mali za uma unaowahusu wateule wake ambao wengi wao wamekosa dira, kujitambua, sifa za uongozi na uzalendo kwa nchi yao na kugeuka kuwa vichaka vya ubadhirifu, wizi na ubinafsi huku wakiendelea kujisafisha kwa kujipakaa madhambi yao kwenye miili yao na kuonekana kama .... 
  
Ninavyofikiri kwa sasa, ni kwamba kunahitajika mabadiliko makubwa ya mfumo wa utawala, uongozi, na wateule waliopo na kupata utawala mbadala, ambao unaweza kuwafanya watanzania wapime na kuwalinganisha waliopo madarakani kwa sasa na wale watakaokuja. Baada ya hapo, nina imani wateule watawajibika kwa wanachi vyema kwani wananchi watakuwa wameshapima na kujiridhisha ya kuwa hawa wanatufaa, na hawa hawafai....

Huu ni mtazamo wa mtu binafsi. Ameutuma ujumbe huu na kuomba niuchape ili watu waupime na kumuunga mkono au kumkosoa. 
  
Happy May Day!

Series: Natures of Our Universe

Wonders of the Nature! Are everywhere. 
 
Recently, when I was flying ...., while we were air-borne on auto-pilot, I just popped out my eyes out of window to get an impression of the blue sky. 
What attracted me was how the appearance of the clouds..... below our aircraft.
  
I had to recall my science knowledge on the forces which maintain the clouds at their position while figuring out what I was seeing out of them. Well, the journey became shorter, and I was glad to arrive at my final destination without being tired despite hours we spent outer there! 
   
Have a blessed monday!

Monday 23 April 2012

CCM Tunawaimarisha kuja kuwa Wapinzani Madhubuti Kwenye Serikali Ijayo - Mbilinyi

Mbunge wa Mbeya Mjini, mh. Mbilinyi amewapa somo wabunge wa CCM ya kuwa wabunge wa CHADEMA kuwapigia kelele wabunge na Serikali ya CCM ni kuwajenga kuwa wapinzani imara mara pale CHADEMA itakaposhikilia dola kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2015. Kwani CHADEMA haitataka kuwa na wapinzani legelege, inahitaji watu wanaoisimamia serikali iliyopo madarakani kwa ushupavu ili wao CHADEMA na serikali yao waende kwenye mstari ulionyooka.


 
Mh. Mbilinyi alikuwa anachangia muswada uliowasilishwa na kamati teule iliyochunguza tukio la kutoroshwa kwa wanayama hai mwaka jana unaohusisha wizara ya Maliasili na Utalii.

  
Taarifa hiyo imejaa kila aina ya takataka utakayoifikiria kutokana na yaliyojiri katika uchunguzi huo.

  
Baadhi ya matatizo yaliyoainishwa ni pamoja na
  • Waziri wa Maliasili na Utalii kujiamulia kutoa vibali kwa makampuni ambayo hayakuomba kibali cha uwindaji
  • Waziri kutoa vibali kwa makampuni ambayo hayakuwa na sifa japo kamati ya ushauri ilimweleza waziri kuwa makampuni hayo hayana sifa
  • Wanyama kusafirishwa wakiwa hai kwenda nje ya nchi bila maombi yoyote kutoka huko nje
  • Raia wa kigeni kupewa kibali cha kukamata wanyama wakati hivyo vibali hutolewa kwa watanzania tu
  • Baadhi ya viongozi wa chama ….. kuingilia shughuli za uhamiaji na kuwapitisha wageni wa shughuli za uwindaji kinyume cha sheria
  • Wanyama kufugwa/kuhifadhiwa kwenye makazi ya watu kwa zaidi ya hata miaka 8 wakati sheria hairuhusu wanyama kukaa sehemu kama hizo au kutunzwa kwa zaidi ya miezi mitatu
  • Vibali vya kukamata wanyama kutolewa kiholela na kwa watu ambao kisheria hawaruhusiwi kuto
  • Vitalu kutolewa bila kufuata sheria zilizopo za uwindaji
  • Kampuni iliyopewa kibali cha kusafirisha wanyama hai ya Jungle International haikuwa imeomba kibali cha kusafirisha wanyama, na pia kimsingi kampuni hiyo ilishabadilishwa jina na kazi miaka mingi na wakati inapewa kibali hicho haikuwapo kwenye daftari la msajiri, kwa maana nyingine ni kampuni hewa.   
Mambo ni mengi na kama una uzalendo na nchi yako unaweza kuivunjilia mbali radio unayosikiliza au runinga unayoitazama.

 

Sunday 22 April 2012

Mnyika Apoza Machungu ya Mh. Omari Nundu

Mh. Omari Nundu

Mijadala ya Bunge letu kwa sasa sio kwamba inaudhi peke yake, bali wakati mwingine inasisimua pia.
Kama watu wengi walivyosikia taarifa ya kamati za Bunge zilizowasilishwa wiki hii, pamoja na taarifa ya mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za serikali ambazo zimeainisha matumizi mabaya ya fedha za uma, pamoja na kila dalili za ufisadi hasa kwa watendaji wengi ambao huwa wanateuliwa na Rais peke yake. 
  
Taarifa hizi zilipokelewa kwa hasira kali na wabunge wote bila kujali itikadi za vyama vyao na hata kufikia maazimio ya kutaka kuleta hoja ya kutokuwa na imani na waziri mkuu iwapo mawaziri waliotajwa kuhusika na kashfa hizo hawatajiuzuru. 
 
Kikao cha Bunge cha jumamosi ya tarehe 21 Aprili 2012, kilidhihirisha mkanganyiko na ugomvi mkubwa uliomo miongoni mwa mawaziri wa serikali iliyopo madarakani, mara baada ya Waziri wa Uchukuzi, Bw. Omari Nundu kueleza bayana ndani ya Bunge ya kuwa hakuwahi kushirikishwa kwa namna yoyote na mkataba unaosemwa upo sasa wa kujenga gati namba 13 na 14 katika bandari ya Dar es Salaam. Alidai ya kwamba kisheria yeye ni mdau muhimu katika kuingia na kuidhinisha mkataba wowote unaohusiana na wizara yake. Kwa maana nyingine inaonekana waziri wa fedha alitumia mamlaka kinyume cha sheria kupitisha mkataba huo bila kumshirikisha Bwana Nundu kama ilivyotakiwa.  
Lakini kwa upande mwingine, naye waziri Nundu, alishindwa kueleza kivipi naye ana mkataba wa "mfukoni" na kampuni nyingine kutoka China, ambapo huo mkataba haujulikani na mtu yeyote isipokuwa yeye peke yake!!!!! 
  
Kikao cha jumamosi kilionekana kuwachanganya watu wote bungeni ikiwa ni pamoja na spika wa Bunge Mama Anne Makinda.

Aliyeokoa jahazi siku ya jana, labda na Taifa kwa ujumla, ni mbunge wa Ubungo, John Mnyika, ambaye alikuja na mapendekezo ya kubadili azimio la kamati inayohusiana na masuala ya uchukuzi ambayo ilitaka gati hilo lianze kujengwa mara moja, ambapo Mnyika alipendekeza upembuzi yakinifu ufanywe na taasisi inayojitegemea. Hii ilitokana na kugundulika ya kuwa mkataba uliopo kwa sasa ulifanywa na kampuni ambayo ndiyo hiyo hiyo ilikuja kupewa tenda ya kujenga gati hilo.
Hali hii ilizusha wasiwasi wa kuwepo na hali ya kuweka makadirio ya juu kupita kiasi na watu kujenga hisia au kuashiria kuwepo na dalili za rushwa ukizingatia makubaliano ya ujenzi hayakuwa na kushindanishwa, ni kama hiyo kampuni ilipewa moja kwa moja tenda ya ujenzi wa magati hayo. 
 
Kilichowafurahisha watazamaji wengi, ni jinsi Bwana Nundu alivyokuwa anashangilia kwa njia ya kibunge baada ya hoja ya Mnyika kuungwa mkono na kupitishwa ambapo ni kinyume kabisa na tulivyozoea kuona kutoka kwa mawaziri ambao mara nyingi hupinga vikali hoja za wabunge wa vyama vya upinzani!

Yaani...... kushangilia kwa mhesh. Nundu......kwangu naona hii ilikuwa ni kama ..... "haya tukose wote"

Tuesday 17 April 2012

Upotoshaji wa Habari za Tanzania

Jana nilikuwa ninasoma jarida la matangazo ya bidhaa za duka kubwa la vitu mchanganyiko (Supermarket) ambalo lilikuwa limenakshiwa kwa picha za kuvutia za bidhaa mbalimbali ambazo ninauzwa katika duka hilo.  
Mbali ya yote hayo, liliongeza baadhi ya habari za nchi za Afrika ya Mashariki ambazo zilijumuisha vivutio mbalimbali vinavyopatikana katika nchi za Afrika Mashariki. 
 
Niliposoma kichwa cha habari kinachohusu Tanzania... nilivutiwa ili nisome makal hiyo.
Kulikuwa na habari nzuri za vivutio kama mlima Kilimanjaro, ziwa Tnaganyika (Lake Tanganyika) na umaarufu wake, pia na bonde la Ngorongoro ambalo ni la kipekee Duniani lilipambwa vizuri.  
 
Tatizo...... 

Nilipoingia kwenye habari za lugha... nilishangaa wakidai ya kuwa lugha ya kigogo ndiyo inayoongewa sana Tanzania ikifuatiwa na kihaya, halafu kiha, tena kimakonde, na wakadai kiswahili hakimo katika lugha zinazo ongewa kwa wingi!!!! 
  
Nilipofika kwenye hoteli na mighahawa maarufu sana ya Tanzania, nilihisi siijui Tanzania....

Nikaona bora niishie hapo na kunywa maji ya baridi, sijui kupoza nini, lakini nilipata nafuu na kuendelea na kazi nyingine. 
 
Kwa anayejua habari sahihi za mambo hayo hapo juu, basi na anifahamishe ili nami niende na wakati!!

Wednesday 11 April 2012

Hofu ya Kutokea Tsunami Yaondolewa


Tetemeko kubwa la ardhi lililotokea leo katika pwani iliyo karibu na Kisiwa cha Sumatra nchini Indonesia ambalo lilikuwa na kipimo cha 8.6 halikuweza kuleta Tsunami kama ilivyobashiriwa hapo awali. 
  
Mawimbi makubwa sana yalikadiriwa kuwa na ukubwa usiozidi meta 1 kutoka usawa wa bahari, na kuna sehemu nyingi walipata mawimbi madogo zaidi na hivyo hayakuleta madhara yoyote zaidi ya usumbufu kwa watu kukimbia na kuingiwa na wasiwasi. 
  
Kufuatia onyo hilo, shughuli nyingi za kwenye bahari ya Hindi zilisitishwa ikiwamo na nchi za ukanda wa pwani ya Afrika Mashariki ambapo ilikadiriwa pwani hii ingeweza kupigwa na mawimbi ya Tsunami hiyo kwenye muda wa kati ya saa 11 jioni hadi saa 2 usiku. 
  
Kutokana na habari zilizotolewa na kituo cha kutoa tahadhari ya Tsunami, ni kwamba Tsunami hiyo haipo tena, na wala watu hawana haja ya kuwa na wasiwasi.

Friday 6 April 2012

Kuenguliwa Kwa Lema, Ndio Mwanzo wa Ukurasa Mpya

Siasaaaaaaaa!
Kuenguliwa Ubunge kwa Godbless Lema kunaashiria mambo mengi, ya kuwa kuna uwezekano wa wabunge wengine nao kun'golewa ikiwa ni pamoja na wale waliopo kwenye baraza la mawaziri la sasa hivi. 
  
Iwapo ukitukana mtu wakati wa kampeni za ubunge wako unaweza kuenguliwa Ubunge hapo baadaye, basi kazi ipo. 
  
Mimi nafikiri tutarajie mengi tu kwenye kesi zinazoendelea. Halafu uchaguzi ukirudiwa, Chama fulani kitashinda.... Wakati huo huo mabilioni ya pesa yatapotea kwenye kampeni, huku dawa na vitendanishi katika hospitali hakuna. 
  
Kweli Bongo akili ipo.
Sitegemei sana mabadiliko ya atakayemrithi Lema, kwani watu wa Arusha hawajabadilika na Serikali yetu tukufu nayo haijabadilika. 
  
Ijumaa Kuu Njema!

Monday 2 April 2012

Matokeo Yasiyo Rasmi: CHADEMA Washinda Arumeru Mashariki

Matokeo yaliohakikiwa na tume ya Taifa ya Uchaguziya katika kata 15 kati ya 17 yameonyesha mgombea wa Chadema, Bw Nassari anaongoza kwa zaidi ya kura 6,000, na matokeo ya kata mbili zizobaki hayatarajiwi kuleta mabadiliko ya ushindi.

Wale waliokokotoa matokeo ya kila kituo, wameshathibitisha ushindi kwa CHADEMA.  
  
Kinachosubiriwa ni kutangazwa mshindi rasmi.  
  
Tahadhari: Haya ni matokeo ya awali.

Matokeo ya Awali ya Uchaguzi wa Ubunge - Arumeru Mashariki

Baada ya kuzuka mvua isiyo ya kawaida ya vurugu na kurushiana mawe imesababisha kucheleweshwa kwa majumuisho ya kura za Arumeru Mashariki, na hivyo kuna uwezekanao matokeo yakatangazwa kukiwa kumekucha tayari.

Fuatilia hapa kura zisizo rasmi za baadhi ya vituo kwa kubofya hapa FK5HA