Member of EVRS

Friday, 24 December 2010

Tanesco! Bado Kabisa!


Shirika la umeme Tanzania (TANESCO) kwa hivi karibuni limeanza kututumka na kutaka kuonyesha kuwa linawajali na kuwaheshimu wateja wake na kuthamini malipo yao kuwa ndio uha wa Tanesco (kwani ndio linawafanya watendaji waweze kwenda haja).
Kumekuwa na vipindi vingi vya kwenye radio na runinga wakijielezea mikakati yao, kujibu maswali ya wasikilizaji na watazamaji na pia kutoa ushauri kwa wenye malalamiko wapi wataweza kusikilizwa.
Hata siku ya tarehe 23 Desemba 2010, waziri wa nishati na madini Mh. Ngeleja akiwa na watendaji wa Tanesco, alikuwa akitoa maelezo na kujibu maswali ya wasikilizaji/watazamaji moja kwa moja (live bila chenga).
Mbali ya juhudi za uongozi wa juu kujaribu kulisafisha shirika hili la ugavi wa umeme, bado watendaji wa ngazi za chini yao, wana roho zilizosheheni kutu, utukutu wa akili au makusudi na kutowajibika.

Kuna sehemu fulani huko manispaa ya Ilala kuna nguzo imeoza na kuegeme ukuta nyumba kwa zaidi ya miaka 3 sasa. Wenye nyumba walishapiga kelele weee mpaka wakamwachia Mungu awalinde hizo nyaya zisijeangukia watu hususan watoto, basi ndio ikawa mauti tena.



Mpita njia waweza kuona nguzo hiyo ikiwa imeegemea ukuta, na kwa hapo chini utaona ule waya unaoshikilia nguzo ikae wima ukiwa umelegea kabisa, kuashiria ya kuwa hauna kazi tena kama ilivyokusudiwa!

Picha hii chini inaonyesha nguzo ikiwa imekwisha kabisa na kugeuka mahali pa ndege kujikinga na jua la Dar es salaam!
Na hii picha juu ndio hali halisi ya nyaya za umeme zikiwa zimeshuka chini kabisa chini ya usawa wa mabati ya nyumba! 

Kinachoshangaza, wiki chache zilizopita, watu wa Tanesco walikuja kumuunganishia umeme mteja mpya, na wakaweka waya kutoka kwenye nguzo hiyo hiyo iliyooza, na walipotaarifiwa kuhusu ubovu wa mlingoti huo, waliuangalia na kusema wanaenda kutoa taarifa ofisini, na kwa sasa inakaribia miezi 2 na hakuna taarifa wala mtu aliyekuja kuona.

Watendaji wa kweli walipotaarifiwa, wakawapa maelekezo walalamikaji mahali pa kwenda na namba za simu, sasa sijui nicheke au... mhusika alipopatikana kwa simu, alisema yupo likizo na akatoa namba nyingine ya mtu ambaye kwa zaidi ya wiki amefunga simu, na watu wakamshauri mlalamikaji ati asubiri sikukuu zipite ndipo akaulizie tena!!!!!

Hivi hizo nyaya za umeme na nguzo zinajua sikukuuu hizo ambazo Tanesco wanasubiri ziishe kwanza!
Na hao wafanyakazi watafungaje line mpya kwenye nguzo wanayoiona imeoza?!
Likitokea janga ... ni nani wa kulaumiwa.
Hakika watendaji wabovu wa Tanesco wanastahili kuongozwa  na mtu kama Stalin :-(

4 comments:

emu-three said...

Mimi sitaki hata kulisikia hili shirika, kama kuna shirika linalochangia kuwadidmiza Watanzania kwenye umasiki ni hili...!

Albert Kissima said...

Dah! Ni masikitiko makubwa. Kama mchezo wa kuigiza vile, hata filamu za kibongo zina uhalisia kuliko utendaji wa shirika hili.

http://abebedorespgondufo.blogs.sapo.pt/ said...

Very good.
Portugal

George, uk said...

hii ni hatari kubwa, sijawahi kuona shirika lililo zembe kama hili. wanachojua ni kukata waya unapochelewa kulipa bili. nafikiri tufike wakati tuwe tunaingia mkataba nao, wakikata umeme kwa sababu zilizo ndani ya uwezo wa binadamu watulipe, nguzo au waya ukileta au kusababisha ajali walipe fidia, nadhani itapunguza uzembe.