Baadhi ya makampuni ya kutengeneza zawadi yameanza kuchangamkia tenda ya kutengeneza zawadi ya Harusi ya mjukuu wa malkia wa Uingereza Prince William ambaye anatarajjia kufunga ndoa na Kate Midleton mwishoni mwa mwezi Aprili 2011.
Kampuni hizo zipo Uingereza na China.
Wamiliki wameanza kutengeneza vito vya thamani kama pete na vyombo vingine vikiwa na picha ya mtoto huyo wa kifalme na mchumba wake, kwani wanatarajia soko litakuwa kubwa sana hapo harusi itakapokuwa inakaribia.
Kampuni moja ya China imeanza kutengeneza pete mfano wa ile ya uchumba ambayo Kate amejipatia. Pete hiyo ambayo imetengenezwa kwa almasi za rangi tofauti tofauti ikizunguka kito cha rangi ya sapphire ilikuwa ya Diana. William alisema hakutaka kabisa marehemu Mama yake apitwe na tukio lolote la harusi hiyo, ndio maana alikubali mchumba wake avikwe pete ambayo ilikuwa ya uchumba ya mama yake.
Wachina wamepata haki ya kutengeneza mfano wa pete hiyo, na kwa yeyote anayetaka kununua, Soko lipo wazi sasa.
Harusi hiyo ambayo itaonyeswa moja kwa moja na vyombo vya runinga mbalimbali inatarajiwa kuvunja rekodi ya harusi kuangaliwa na watu wengi duniani.
Gonga hapa kupata habari zaidi
5 comments:
Tenda tenda hizooo. Wengine bado tumelala!
Lakini maharusi hayo ya kifahari yanadumu kweli? Lakini ndio hivyo kila mtu hujikuna pale anapofikia au sio! Twawatakia harusi njema!
Hamna hata kwenda kazini wala shule siku hiyo kaka chib!!!! hahahaaaaaaa!!! Ila watadumu...unless amuue msichana na wa watu...I am sorry that was a bad joke
kwikwikwikwikwi
natamani dunia hii ingekuwa na ufalme wa kweli, nami ningeulilia, yaani mpaka chib wa rwanda muchiduba anaongelea harusi hii?
Nawasiwasi na MAANA YA HARUSI siku hizi !:-(
Post a Comment