Member of EVRS

Tuesday, 5 October 2010

Ziara Fupi ya Arusha - Nairobi - Kigali kwa siku Moja


Last week I visited Arusha town, after more than 3 years without stepping my feet to this beautiful city.
It was dusty, and after walking about, I noted my shoes were powdered by vumbi!
I visited one of the shoe shiners ( Jamani hii kazi imekodiwa na wachagga), while waiting for my shoes to be ready, alas! I was given makata mbuga to wait while protecting my socks from dust.
Makata Mbuga, are local sandals, famously know as "Arusha to Moshi" by people living in this area. They are made from rejected or old car tyres. Maasai version of makata mbuga are more interesting!
The city  is beatiful and clean, at least to the areas I visited
Lakini.. when you go to Ngaramtoni, yaani ongeza sponji kwenye kiti, na chunga sana kichwa chako, kwani barabara ipo kwenye mashimo, na sio mashimo yapo kwenye baarabara.
Habari mpya nilikutana nayo njiani wakati Naelekea Namanga wakati wa asubuhi baada ya chai, kwani kuna baba mmoja wa kimasai, tulimkuta ana kijana mdogo wa kiume kama miaka 7 hivi kavalia sare za shule siku hiyo ya jumapili!!
Tulisimama, akasema, ero sopai!, nami nikajibu sopai orubaiyan, akaomba....saidia napeleka mutoto panado, yeye anasuka kuni boma ya ... ole parkw..., na mutoto yeye najua kabsaa, .. eeeh , tukamalizia kwa ashee, ashee nale. Naye akawahi kurudi kwa sangiki yake.
Kusema ukweli, huyo baba anajua umuhimu wa elimu, wikendi mtoto anarudi nyumbani, jumapili anawahi tena asubuhi, kwani shule ipo kama km 12 kutoka kwenye boma ya huyo baba, na aliposhukia ni porini..., kama kilomita 2-3 kufika shuleni kwao (Longido mjini).

Mchana, nilikuwa Nairobi, baada ya lunch, nilichukua taksi, kwa jinsi dereva alivyokuwa anaongea, na mate yanaruka kupitia geti la chini(Mwanya wa kutengeneza kwa kung'oa meno ya chini), hakika ni mluo, akadai pale nilipomkuta haparuhusiwi madereva wa kabila jingine, na hasa wakamba, ati wakienda kupaki pale ni nuksi, na kuna mkuu wa polisi fulani anawakingia kifua kwa ukorofi huo. Kwa kuwa alikuwa peke yake, akawa na wasiwasi watakuja kupaki, hivyo alinikimbiza airport kama mbio za langalanga, I had to ask him if he has helmet!!!, kwani mkanda niliona hautoshi, nikihofia kupata head injury kama atakutana na hump, kwani naweza kurushwa kwenye roof, anyway niliwahi airport, kwani nilikuwa karibu kuchelewa!!!

Usiku, nilifika Kigali, dereva wa taksi aliingia mitini, ati alisikia baridi pale airport na ndege yetu ilichelewa kwa dk 45!!, bahati nilipata usafiri wa mabasi yanayopaki karibu kabisa na airport ambayo yalikuwa hayana watu wengi, kwani nilikuwa na kimkoba kidogo tu, na kulikuwa hakuna taksi. Nikamaliza safari yangu kwa kupanda mabasi mawili hadi kufika kiotani kwangu, na yote yakiwa na makonda wanawake/wasichana, wakihangaika kupiga debe kila kituo! Ila wenyeji walikuwa wanayakwepa kwa kuwa yana ongezeko na pesa zaidi kidogo kuliko yale ya kawaida.

Sheeee

8 comments:

EDNA said...

Makatambuga yamekutoa kwelikweli.And i heard that Arusha is one of the expensive city in Tanzania....Is that true kaka?

chib said...

Da Edna.. ha ha haaaa, mimi mwenyewe nilikuwa najishangaa ati.
Enzi hizo wakati naishi Arusha, nakubali nilikuwa nauona mji huo ni ghali, lakini majuzi nikitokea Kigali, niliuona ni nafuu baada ya kuwa nimeleweshwa na gharama za juu za Kigali.

Cris said...

Curious sandals and place.
Hugs!

Anonymous said...

Thank you for this interesting journey.
Remember in the North of Spain to have seen nearly alike shoes. May time and life treat you all kind.


daily athens

emu-three said...

Wau, wau, ...makatambuga...nafikiri kuna haja ya kuviboresha viwekwe kimtindo wa viatu , ...vinadumu, na vinahimili shughuli za mbugani zenye miba...na kwa bongo-dar, zitasaidia sana kwenye msukumano ndani ya daladala, ukikiweka mguuni mwa mtu, atakupisha tu...yallah unanikanyaga...mmmh

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

napenda sana kuvaa hii kitu ila tatizo waifu hapendi nivae!!!! eti ni noma harafu safari yako hiyo duh!! natamani ndege iweje sijui

chib said...

emu 3 na Kamala, ha ha haaa, si munamuona jamaa wa ugiriki naye anadai huko uhispania kuna watu wanavaa.

Subi Nukta said...

jana nimecheka sana niliposoma kisa hiki, wewe ni msimulizi mzuri, mtani na mcheshi.