Member of EVRS

Friday, 10 September 2010

Sikukuu ya Idi na Kazi

Picha: Mmachinga wa huku akiwa kazini akiuza vifaa vya wapenzi wa Urastafari kama alivyo onekana mtaani leo.


Leo ni sikukuu ya Idi.
Hapa Kigali ilikuwa ni siku ya mapumziko, nasikia kwa hapa inasheherekewa kwa siku moja tu.
Tofauti niliyoiona ni kuwa ofisi za serikali, mabenki na maduka machache ndio yaiyokuwa yamefungwa.
Sehemu kubwa ya wafanya biashara walikuwa kazini kama kawaida.
Waislamu kwa hapa Rwanda ni wachache sana.
Eid Mubarak!

Wednesday, 8 September 2010

Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara Kigali, Rwanda - 2010

Leo ilikuwa ni siku ya mwisho ya maonyesho ya kimataifa ya biashara hapa Rwanda maarufu kama EXPO 2010 yaliyokuwa yakifanyika katika viwanja vya Gikondo.
Nchi mbalimbali zilishiriki zikijumuisha nchi zote za Afrika mashariki na nyingine kutoka nje.
Kwa wengine tumeweza kufaidi kupata bidhaa za nyumbani Tanzania kwa bei ya nyumbani, kwani mara nyingi bidhaa za Tanzania kwenye soko la huku ni ghali, kwani zinaheshimika ya kuwa na ubora wa hali ya juu. Wananchi wakigaguliwa na askari kabla ya kuingia viwanjani, ni upekuzi wa kupapasa mwili wote usije ukawa umebeba silaha na kuleta vurugu
Kuelekea lango kuu la kuingia kwenye maonyesho kwa ndani

Baadhi ya bendera za nchi washiriki

Kibanda cha jadi kilichokuwa na mvuto. Sharti la kuingia ndani ya banda ilikuwa ni lazima kuvua viatu na kuviacha nje kwenye lango la kuingilia humo. Nafikiri wale wapenzi wa kutembea na soksi zilizotoboka, na miguu isiyo oshwa walikuwa wanakiona kibanda hiki ni sumu kwao.



Tuesday, 7 September 2010

American Pastor to create Havoc in Islamic World?

Pastor Terry Jones of a small church called Dove World Outreach Center in Gainesville, Florida has a strong impulse to burn the moslem holy book - Koran to mark the rememberance of September 11 attack at WTC twin towers.

He has been warned by the commander of armed forces in Afghanistan General David Petraeus not to do so, because of the after effect reaction in the moslem world as a result of what he is intending to do. But it seems he is not convinced to stop his plans.

Read here

Monday, 6 September 2010

Kagame aapishwa kuwa Rais wa Rwanda

Rais Kagame wa Rwanda ameapishwa leo kuwa Rais kwa muhula wa pili.
Sherehe hii ilihudhuriwa na viongozi wa nchi mbalimbali kutoka nchi kadhaa za kiafrika.
Baadhi ya viongozi hao ni kutoka Burkina Faso, Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, Afrika ya Kati, Kenya, Malawi, Ethiopia, Liberia n.k.


Kagame akila kiapo leo.
Rais Kagame akisaini hati ya kiapo huku aiangaliwa na jaji mkuu wa Rwanda Aloysie Cyanzaire


Gwaride lililokuwa limeandaliwa mahsusi kwa shughuli ya leo kwenye uwanaja wa Amahoro.


Katika hotuba yake, Rais Kagame aliwashukuru viongozi wa kiafrika kwa kukubali mwaliko na kuonyesha mshikamano wao. Pia aliwashukuru wanyarwanda kwa kuchagua serikali ambayo wanaona itakidhi matakwa ya maendeleo ya wanyarwanda.
Lakini alikemea vikali tabia za baadhi ya mashirika ya kimataifa na haki za binadamu kwa kuamua kwa makusudi kupotosha ukweli wa amani iliyopo Rwanda, na kuamua kutangaza propaganda za uongo kuhusu hali iliyopo Rwanda kwa sasa.

Alionyesha kushangazwa kwa mashirika hayo kutozingatia hali halisi ya kisiasa ya Rwanda katika kipindi hiki cha mpito baada ya mauaji ya kimbari ya mwaka 1994.

Mwisho alisisitiza ya kuwa hakuna maendeleo yanayokuja bila kuwa na demokrasia (Hiki ni kijembe kwa wale wanaoisifia Rwanda kuwa na maendeleo makubwa sana na huku wakisema hakuna demokrasia kabisa). Na aliyakemea mashirika hayo kuwa yanataka kuchochea gurudumu la umaskini na maendeleo duni kwa nchi zinazoendelea kama Rwanda ( Perpetuates cycle of poverty and underdevelopment).

Alionya ya kuwa Rwanda kamwe haitakubali kuamriwa cha kufanya kama Taifa, akiwa na maana utaifa na mahitaji ya Rwanda ndio yanayopewa kipaumbele.


Quot from Kagame: A successful society, achieves National cohesiveness and common interests.

Hotuba hii ilinigusa sana, hasa ukizingatia juzi nimepokea taarifa ya kuwa kuna mashirika tajiri, eti kwa kuona kuna uhaba mkubwa wa madaktari wa fani fulani za magonjwa katika nchi za kiafrika, basi wanataka kuelekeza misaada yao ambayo walikuwa wakiitoa kwa kutoa mafunzo kamili ya udaktari kwenda kuwafundisha watu watakaowaokota mitaani na kuwapa mafunzo mafupi ya kutibu watu ikiwa ni pamoja na upasuaji ili waongeze idadi ya "madaktari" wa fani hizo katika nchi za kiafrika. (J*^ga kabsaaa)
Nikiwa mmoja wa wadau katika fani hizo zenye upungufu, tuliombwa kutoa mapendekezo kama kipima joto, ingawa wao ati walishakubaliana. Nahisi joto wamekwishalipata.

Picha kutoka Kagame fan club

Sunday, 5 September 2010

Rwanda: Paul Kagame Kuapishwa Kesho Muhula wa Mwisho

Kesho, kutakuwa na sherehe ya kuapishwa kwa Paul Kagame kuwa rais kwa kipindi chake cha mwisho cha urais cha miaka 7. Hii ni kwa mujibu wa katiba ya sasa ya Rwanda.
Kwa ujumla Kagame bado anakubalika sana na wanyarwanda. Pichani juu: Katikati ya Jiji la Kigali kama linavyo onekana wakati wa jioni kutoka nyumbani kwangu.

Tangu mwezi wa nne, kumekuwa na marekebisho makubwa ya bararbara ikiwa ni pamoja na upanuzi kwa kuongeza njia mbili kwenye baadhi ya barabara ambazo zilikuwa na msongamano wa magari, na pia barabara zilizokuwa zimeanza kuonyesha dalili ya kuanza kuchakaa, hasa zile barabara maalumu zinazopita kwenye ofisi za balozi na wizara za serikali


Wajenzi ni wachina, lakini hawa sio wale feki, kwani wanafanya kazi kwa makini na kwa haraka, sio kama wale waliotengeneza barabara ya Sam Nujoma kule Dar es Salaam.

Wachina hawa, wana imani kubwa na sementi ya Tanzania, kwani katika ujenzi wa sehemu za wapita miguu, mitaro na kusimika nguzo za taa za barabarani wanatumia sementi pekee ya Twiga kutoka Dar es Salaam, Tanzania.



Shughuli ya kuweka lami mpya ilikuwa inaenda sambamba na kuweka taa mpya na kuondoa za zamani, ambazo baadhi yake zilikuwa haziwaki, lakini wamebadili zote kabisa hasa barabara muhimu.
Kwa sasa barabara zimekamilika na wamemaliza kupaka rangi kingo za barabara ili zionekane kwa madereva kwa urahisi na pia kupanda miti na maua.
Kesho ni siku ya mapumziko, lakini nahisi jumanne nayo inaweza kuwa mapumziko iwapo watu watasheherekea sana kuapishwa huko kwa rais Kagame, kwani watu hupenda kukesha usiku kucha kwenye uwanja wa Taifa wa Amahoro, hivyo kushindwa kufanya kazi siku inayofuata.


Saturday, 4 September 2010

Algeria 1 - 1 Tanzania for AFCON 2012 Qualifying Race

Tanzania managed to hold the host Algeria 1 - 1 at an encounter which was dominated by the Desert Foxes - Algeria.

Algeria which is superior to Tanzania in FIFA ranking, fails to score many goals on several opportunities they got. Thanks to Tanzanian goalkeeper who saved numerous number of what was looking to go inside the net.

All goals werescored in the first half, Tanzania got the goal in 34th minute, and Algeria equalised at 45th minute.

Algeria still is facing hard time for the 5th game in a row without any win, and have scored not more than 1 goal among the 8 games they have played so far including today's match.

Tanzania similaly, hasn't won in their last 6 games, but at times had managed to score more than one goal in a match.

Prior to this match, Tanzania coach declare that his team will fight to the last nail knowing they are going to face tough opponents, and he was determined to come out with one point, or even three!

His dream came out true!

Friday, 3 September 2010

Vurugu za Mikate Msumbiji!


Juzi usiku nilikuwa naangalia TV Mozambique kupitia satellite dish.

Kwa kuwa sielewi kireno, nilibaki nikishangaa kuona watu wanaume kwa wanawake tena wa rika zote wakivamia maduka na kuiba kila kitu kilichokuwepo, na huku barabarani vijana wa kiume wakichoma matairi ya magari.

Nilimshuhudia dada mmoja labda akiwa kwenye miaka kama 20 hivi akitoka na mabeseni kama 10 hivi kwenye duka lililovamiwa huku akikimbia akiwa na tabasamu usoni. Hakufika mbali kwani alivamiwa na kundi la vijana wa kiume wakiwamo na watoto kama wa miaka 12 – 13 wakampokonya mabeseni yote huku wakimwachia majeraha makubwa kichwani na usoni na huku akiwa tayari kagalagazwa chini.
Yote hii ilikuwa ni purukushani ya kumnyang’anya mabeseni ili na wao wajipatie. Kilichofuatia ni kilio na kicheko kikafutika kabisa usoni pake.

Pia niliwaona akina mama wa makamo na akina baba pia wakiiba unga kwenye duka la vyakula na kukimbia!

Jana ndio nikapata jibu kuwa waliamua kufanya fujo baada ya serikali ya Msumbiji kupandisha bei za vyakula. Lakini kilichowakera zaidi ni kupandisha sana bei ya MIKATE!!!

Polisi waliingilia kati na kufyatua risasi za moto. Vurugu hizi zimesababisha vifo vya watu 7 na wengine kadhaa kujeruhiwa.

Pamoja na kuwa hali leo asubuhi imeanza kutengemaa kidogo, ingawa bado usafiri wa wananchi haujarudi sawasawa, serikali ya Msumbiji imetamka ya kuwa haitapunguza ongezeko la bei kama ilivyokuwa imeahidi jana kwamba itapitia upya.

Swali kubwa…. Tunaelekea wapi sisi nchi za Kiafrika? Je, sera za serikali zetu zina angalia hali ya wananchi kabla ya kufanya maamuzi au…?

Kwangu siamini kuwa suala la kupandisha bei ya mikate tu ndio inaweza kuleta vurugu kama hizi.

Habari za kina click here

Photo: By Reuters

Thursday, 2 September 2010

Dr. Faustine Ndugulile Anaomba Kura Yako

Dr Faustine, mwanablogu mwenzetu, ameingia kwenye kinyang'anyiro cha ubunge jimbo la Kigamboni Dar es Salaam.

Ana ujumbe mfupi tu kwa wana-Kigamboni.

Anawaomba kura zao ili waweze kushirikiana pamoja kutatua kero zinazowakabili ili kuleta maendeleo ya kweli kwa Kigamboni.