Member of EVRS

Wednesday, 8 September 2010

Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara Kigali, Rwanda - 2010

Leo ilikuwa ni siku ya mwisho ya maonyesho ya kimataifa ya biashara hapa Rwanda maarufu kama EXPO 2010 yaliyokuwa yakifanyika katika viwanja vya Gikondo.
Nchi mbalimbali zilishiriki zikijumuisha nchi zote za Afrika mashariki na nyingine kutoka nje.
Kwa wengine tumeweza kufaidi kupata bidhaa za nyumbani Tanzania kwa bei ya nyumbani, kwani mara nyingi bidhaa za Tanzania kwenye soko la huku ni ghali, kwani zinaheshimika ya kuwa na ubora wa hali ya juu. Wananchi wakigaguliwa na askari kabla ya kuingia viwanjani, ni upekuzi wa kupapasa mwili wote usije ukawa umebeba silaha na kuleta vurugu
Kuelekea lango kuu la kuingia kwenye maonyesho kwa ndani

Baadhi ya bendera za nchi washiriki

Kibanda cha jadi kilichokuwa na mvuto. Sharti la kuingia ndani ya banda ilikuwa ni lazima kuvua viatu na kuviacha nje kwenye lango la kuingilia humo. Nafikiri wale wapenzi wa kutembea na soksi zilizotoboka, na miguu isiyo oshwa walikuwa wanakiona kibanda hiki ni sumu kwao.



5 comments:

Simon Kitururu said...

Na nukuu ``Bidhaa za Tanzania kwenye soko la huku ni ghali, kwani zinaheshimika ya kuwa na ubora wa hali ya juu.´´- mwisho wa nukuu.

Watanzania WENYEWE wangekuwa wanaheshimu bidhaa za Tanzania ndani ya Tanzania - ingekuwa bomba sana .

Paragrafu ya mwisho imeniacha hoi. Maana kuna watu wakivua kiatu ni balaa maana mpaka mbu wanakufa na inzi wanatoka baruti kisa harufu imezidi.:-)

kamala Lutatinisibwa Lutabasibwa said...

mhhhhh soxi za chib zinanukaaaaa

Anonymous said...

Simon na Kamala ha ha haaa, mimi nafikiri waliokuwa na matatizo ya miguu wamesimama hapo nje ya kibanda

John Mwaipopo said...

inawezekana ni aina ya siment. sio kama wanaiheshimu ila haipatikani nyingine. kuna aina ya simenti haifai kujengea majengo makubwa makubwa. kwa mfano hapa mbeya kuna kiwanja cha ndenge cha kimataifa kinajengwa. kinapojengwa ni upenuni mwa kiwanda cha tembo simenti. lakini simenti inayotumika kujengea ni ya kiwanda cha wazo cha dar es salaam. tembo simenti inatengenezwa kwa madini yaitwayo pozolana. hii inafaa kwa hizi nyumba zetu na vitu visivyo vikubwa. sidhani kama hao wajenzi wanatumia simenti yoyote kutoka tanzania. lazima watakuwa wanatumia ya dar au ya tanga zote zinafaaa kwa maujenzi makubwa makubwa

chib said...

@ Mwaipopo. Nashukuru kwa ufafanuzi.