Umoja wa Watanzania wanaoishi Rwanda unapenda kuwaalika watu wote katika hafla ya chakula na dansi katika kusheherekea miaka 50 ya uhuru wa Tanzania Bara (Tanganyika).
Sherehe hizi zitafanyika tarehe 9.12.2011 jijini Kigali. Siku kama hiyo miaka 50 iliyopita ndipo Tanganyika ilipopata uhuru kutoka kwa wakoloni wa Kiingereza.
Mbali ya chakula (Chenye asili ya Kitanzania) na dansi, kutakuwa na maelezo mafupi ya historia ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambao ndio uliozaa jamhuri ya Muungano ya Tanzania.
Watu wote mnakaribishwa kwa kiingilio kidogo cha faranga za Rwanda 8,000 tu.
Mawasiliano kwa waratibu yameandikwa kwenye kadi za mwaliko.
KARIBUNI SANA!
1 comment:
Duh! naona ntashindwa kuhudhuria ila nawatakieni kila la kheri wote mtakaotuwakilisha.
Post a Comment