Member of EVRS

Friday 23 September 2011

Chama cha Upinzani Chashinda Uchaguzi Mkuu wa Zambia

Chama cha Upinzani  nchini Zambia, Patritic Front kimefanikiwa kupata ushindi wa urais pale bwana Michael Chilufya Sata (Miaka 73) alipotangazwa kuwa mshindi wa uchaguzi wa Rais wa nchi hiyo.
Ukiwa ni msimu wake wa nne kwa bwana Sata kugombea nafasi hiyo, safari hii amefanikiwa kumshinda bwana Rupiah Banda, ambaye ndiye alikuwa anashikilia wadhifa huo.  
  
Uchaguzi huu kwa mara ya kwanza ulileta tafrani ambayo ilisababisha Tanzania, ambao ni nchi jirani na Zambia kwa upande wa kaskazini, kufunga mpaka wake na Zambia kuepusha wimbi la wakimbizi na waleta fujo kuingia Tanzania bila mpangilio. 
 
Sata amepata jumla ya 43% ya kura zote halali zilizopigwa, akifuatiwa na Bwana Banda aliyepata 36% ya kura zote halali zilizopigwa. 
  
Ninahisi ya kuwa uchaguzi huu wa Zambia utakuwa umetoa funzo fulani kwa siasa za kiafrika na hasa nyumbani kwetu Tz na nchi nyingine kama Zimbabwe na Uganda.  

No comments: