Matokeo ya kidato cha nne mwaka 2010 kusema ukweli ni ya aibu tupu!
Kiwango cha kufaulu na kufeli vimekaribia kulingana, kwani si kitu cha kujivunia hata kidogo iwapo karibu nusu ya watahiniwa wanaambulia daraja ziro (division zero)
Kilichochangia zaidi ni kuanzisha shule kisiasa bila kuandaa waalimu wa kufundisha katika shule hizo. Ndio maana tumeshuhudia matokeo mabovu kabisa.
Hii ni changamoto kwa watu wote, na pia kwa wale watu ambao wamekubali shule zitumie majina yao, wana wajibu wa kuzisaidia shule hizo kupambana na matatizo wanayokutana nayo.
Ifuatayo, ni baadhi ya mifano ya shule zilizochemsha kama nilivyonukuu kutoka kwenye tovuti ya baraza la mitihani kwa matokeo ya kidato cha nne 2010:
Shule Daraja 1 - 2 - 3 - 4 - 0
Anna Mkapa 0 - 3 - 11 - 69 - 109
Karamagi 0 - 0 - 0 - 11 - 6
Celina Kombani 0 - 0 - 1 - 21 - 44
Mary Nagu 0 - 0 - 0 - 18 - 36
Felix Mrema 0 - 0 - 4 - 38 - 118
Prof Philemon Sarungi 0 - 0 - 0 - 19 - 52
Balozi Mshangama 0 - 0 - 0 - 8 - 33
Kabwe 0 - 0 - 1 - 18 - 23
J. M. Kikwete 0 - 4 - 2 - 29 - 52
Mwanamwema Shein 0 - 0 - 4 - 27 - 66
Salma Kikwete 3 - 8 - 27 - 119 - 150
Mwapachu 0 - 0 - 1 - 27 - 171
Monica Mbega 0 - 0 - 0 - 3 - 31
Nyamoko 0 - 0 - 2 - 51 - 52
Chokocho 0 - 0 - 0 - 13 - 42
Ukonda Moyo 0 - 0 - 1 - 9 - 31
Mswaki 0 - 0 - 2 - 10 - 27
Kilamacho 0 - 0 - 2 - 35 - 89
Mabwerebwere 0 - 1 - 1 - 7 - 56
Ukata 0 - 0 - 0 - 9 - 54
Mtumba 0 - 1 - 0 - 18 - 60
Shume 0 - 0 - 5 - 39 - 102
Dindira 0 - 0 - 0 - 21 - 84
Mwisho wa Shamba 0 - 0 - 0 - 28 - 97
Zuzu 0 - 0 - 0 - 3 - 19
Napenda kuishia hapa, kwani orodha ni ndefu, na inaweza kukufanya ukapata ugonjwa wa moyo!
9 comments:
Duuuh, kweli heri uishie haapo, maana naona majina ya shule za waheshimiwa...mh, sijui wenyewe wakiangalia wanajisikiaje, ichukuliwe yeye mwenyewe alipiga one ya nguvu!
Mimi najiuliza, hawa wahitimu asilimia 89 wataishia wapi? Maana ni wazi hawatendelea na masomo! Huko watakakokuwa, watakuwa watu wa aina gani?
Walipoambiwa miaka minne iliyopita kwamba na wao wako shule, je leo hii baada ya uozo huu wanaweza kuamini hivyo(kwamba walienda shule)? Wataipenda serikali na chama chake kama inavyotaka yenyewe?(maana wengine tunaambiwa walikuwa wanaandika matusi kwa serikali badala ya kujibu mtihani)!
Shule nyingine zina majina ya kukata tamaa!
Anony, si wajua kuna sekondari zaidi ya 3,000. Nahisi majina yalikuwa yamekwisha, japo kwa kufikiria haraka haraka
Have a wonderful weekend :-)
((hugs))
Naam, ni aibu kwa Taifa, aibu kwa walimu, aibu kwa wazazi/walezi na pia ni aibu kubwa kwa wanafunzi. Makundi yote haya yanahusika na matokeo haya mabovu.
Mbali na hali duni(kukosekana kwa waalimu, mazingira duni ya kusomea na kufundishia, n.k) ya shule zetu, hususani za kata (kwani zipo hata za binafsi zilizo na mazingira hovyo kabisa ya kusomea na kufundishia) pia, wanafunzi walio wengi wanasumbuliwa na tatizo kubwa la kutokujitambua. Wawapo katika hali duni hizi za shule zetu, hawaoni wala kujua kuwa mazingira yale ni changamoto kwao, wanapoteza muda mwingi kufanya mambo yasiyo na tija. Hawaoni hata umuhimu wa kutumia vyema nafasi waliyoipata ya kupewa vituo vya kufanyia mitihani. Wamekuwa wakorofi tu mitaani, fesibuku kwao imekuwa fasheni, wanajihusisha na ngono zembe na mambo chungu nzima yasiyo ya kimasomo wala kimaendeleo. Juhudi kubwa wanaielekeza kwenye mambo haya kuliko masomo. Hii ni sehemu ya chanzo cha tatizo.
Wazazi/walezi , walimu, serikali na taifa kwa ujumla, mbali na juhudi zao wenyewe, wengi wa wanafunzi hawa wawezeshwe KUJITAMBUA ili mwishowe wafahamu nini wanatakiwa kufanya (wao kama wanafunzi) wanaokabiliwa na hali ngumu ya mazingira ya kusoma na kufundishia.
Labda tujiulize, hawa wanaopata div 1 ktk mazingira haya haya ya div 0 na 4, wana nini cha ziada? Tunaweza kusema wanazidiana uwezo kiakili, lakini uwezo huu wanauonesha/wanautumia katika mazingira tofauti na wengine?
Wazazi tumejenga shule za kata wenyewe, kwa nguvu zetu, hatuna budi kuhakikisha shule hizi zinakamilika. Tuendeleze michango na kutafuta ufadhili, kwa juhudi zetu, tuhakikishe kuna maabara zenye vifaaa vya kutosha, kuna maktaba yenye vitabu muhimu, kuna nyumba bora za walimu na hata kuchanga fedha kwa ajili ya kuwalipa walimu zaidi ya mshahara wa serikali, binafsi naona tuna wajibika kwa haya. Tukiisubiri serikali, watoto wetu wataendelea kupoteza muda wao bure na kufanya wakachukua mikondo isiyowafaa katika maisha. Hili naliona (pamoja na mambo mengine mengi) pia ni sehemu ya suluhisho.
Thanks Albert, Mchango wako ni mkubwa na muhimu sana
DUH ! Jamani nimekosa hata la kusema!:-(
Jamani hili suala la elimu yetu nimelipigia kelele hadi nimechoka. Nimeandika articles hadi kwenye magazeti lakini nani anajali. Mfumo wetu wa elimu umepitwa na wakati. Viongoze wetu inabidi wajifunze kutenganisha taaluma na siasa.
Raisi wa nchi anakuambia kilimo kwanza badala ya Elimu kwanza. Hiyo ndiyo slogan ya Mheshimiwa Rais Dr......... Sasa hapa tutegemee nini!
Post a Comment