Sunday, 15 May 2011

Fahari au Utumwa wa Kublogu

Kazi ya ku-blogu si ndogo kama wapenzi wa kusoma blogu wanavyofikiria. 
  
Kila siku lazima utafute jambo ambalo litawapa habari mpya wasomaji wako au kuwaburudisha.
Na kama unataka kuwasiliana na watu au kujua nini kinachoendelea kwenye mitandao ya kijamii, basi ni lazima uwe na laptop, kamera ya kunasa matukio, simu yenye uwezo wa kupokea taarifa mbalimbali na nyenzo za kuhamisha taarifa hizo kutoka kwenye kinasio cha kwanza na kwenda cha pili. 
  
Mbali ya yote hayo, kuna gharama za kutumia simu au internet, na pia muda wa mtu binafsi, wakati mwingine unalazimika kula huku ukiwasiliana na kupata habari za watu wengine. 
 
Kaka Fadhy... upoooooo!

14 comments:

  1. nipo kaka...nimekuwa kimya kwa kuwa hizo nyenzo zote ulizozitaja hapo, wajanja waliniibia kwa mkupuo. Nikawa nashindwa kublog. Ila sasa narudi kublog.

    Ahsante sana kaka kunikumbuka.

    Kublog, mie sijui niiteje? Utumwa si utumwa. Ila ni kama ulevi fulani hivi. Ukishakuwa addicted, ukikosa unahisi unaugua na kuugua.

    Ila kublog ni raha, nikiazima maneno ya kaka Mubelwa, "uwafunzao ndio wakufundishao".

    ReplyDelete
  2. Kila jambo jema lina gharama, ndio maana nikapenda huu usemi usemao;

    `Kama elimu gharama, hebu jaribu ujinga.

    Kwanini nikaweka usemi huu,ambao unaweza usionekane kuwa ni mahala pake: ni kwamba jema huwa twaliona lina gharama, kama wema uilivyo na mitihani ! Lakini tija yake ni kubwa kuliko hiyo gharama!

    Mkuu tupo pamoja na kweli kazi hii ina mitihani, gharama, muda na mwisho wa siku unaweza ukakata tamaa, lakini tija yake ni kubwa sana. Mungu mwenyewe ndiye anajua.!

    ReplyDelete
  3. chib nilisikia unataka kulipwa kwa kazi yako hii!! umechemsha

    ila sasa kuna wajanja wanatumia blogu zetu kupeana awards

    ReplyDelete
  4. Nakubalina na mtani Fadhy kuwa kublog ni kama ulevi fulani vile. Pia ni kwamba katika hizi blog tunajifunza mengi sana na kuna wengine wanaandika vitu ambavyo wangeweza kuandika vitabu ambavyo wengi wangesoma na kuelimika sana. kwa hiyo kublog si UTUMWA kwa vile hakuna anayetulazimisha. Halafu hapo hapo unapata marafiki ambao hukutegemea kabisa. Na kaka Chib nilikumiss kweli kaka KARIBU SANA:-)

    ReplyDelete
  5. @Fadhy: Unajua umejibu kilichokuwa swali langu hasa kuhusiana na kuona haupo sana siku hizi kikublogua!

    Mengine kanisemea Yasinta!

    ReplyDelete
  6. Mtakatifu Simon, nilivamiwa na majambazi wenye silaha wakanipora gari, ndani kukiwa na viblogio vyote. Laptop, kamera, modem na simu ya mkononi. Hivyo nikabaki kama nilivyo. Kama ujuavyo, hali kama hiyo hata hamu ya kwenda cafe kublog sikuwa nayo. Ni mwezi sasa, nikaona nirejee jamvini. Namshukuru Mungu kwa uhai.

    ReplyDelete
  7. Pole sana mkuu kwa mkasa huo, sijui tuutungie kisa nini, tutawasilina mkuu unitonye ilivyokuwa...
    Kweli wewe u mpiganaji halisi maana umepitia misukosuko ...POLE SANA MKUU!

    ReplyDelete
  8. Halafu asiyejua hata kuweka HTML Link ya ku"open new window" anakuja kunitajia ni nani anayefanya kazi bora as a blogger.
    Yaaaaaaaniiiii

    ReplyDelete
  9. Fadhy pole sana, sikuwa na habari ya kuwa hao jamaa walikukumba, nilichokuwa nashangaa ni ukimya.
    Wakati mwingine ukibaki mzima unamshukuru Mungu.
    Achana na taabu zote za kublogu, lakini inasaidia sana kufahamiana na watu wengi muhimu katika maisha yako, na pia habari nyingi mbalimbali ambazo hukutarajia kuzijua, na pia mmiliki wa blogu, akili inachangamka na kufikiri kesho nifanye nini, kuliko kukaa tu kama mkosa yote.
    Nilitoa mada hii na picha ya Fadhy makusudi kumchokoza nijue kulikoni!
    @ Kamala, nashukuru ujumbe wako umefika, najua unawalenga hao wanaotumia kazi zetu kupeana awards, kwangu kublogu ni kama mtu napoamua kukaa barazi na kupunga upepeo, hakuna anaytarajiwa kulipwa kwa kupunga upepo
    @ Da Yasinta, ahsante, nipo ila nimebanwa na hitimisho la masomo, namalizia malizia kuandika thesis, kaaaazi kweli kweli.
    Wengine, bila kutaja majina ahsanteni kwa mawazo yenu. TUPO PAMOJA

    ReplyDelete
  10. Samahani, nje ya mada kidogo:

    Hebu pita hapa: http://changamotoyetu.blogspot.com/2011/05/majibu-ya-mmiliki-wa-tuzo-za-blog.htm

    Au pia hata hapa:http://kamalaluta.blogspot.com/2011/05/wanaotoa-tunzo-za-bloggers-na-watoe-kwa.html

    Na usiishie hapo kuna hapa pia: http://mtayarishaji.blogspot.com/2011/05/majibu-ya-mmiliki-wa-tuzo-za-blog.html

    Mwisho pia kuna hapa: http://bwaya.blogspot.com/2011/05/wanablogu-wanasemaje-kuhusu-utaratibu.html

    NINA UHAKIKA HAUTAKOSA LA KUSEMA KULINGANA NA UTAKAVYOLITAZAMA JAMBO LENYEWE.

    ReplyDelete
  11. Kaka Fadhy Mtanga pole sana kwa yaliyokukuta, Tunamshuru Mungu kuwa wamekuachia uzima, vingine utapata tuu!Ubarikiwe sana na asante kwa kaka Chib kwa kuchokonoa haya mpaka kujua kulikoni.

    ReplyDelete
  12. @Fadhy: Pole sana Mkuu!

    Nchi yetu iitwayo ya amani hiii we acha tu!:-(

    Tunashukuru Mungu lakini wamekuachia Uhai!

    Polisi katika tukio kama hili sijui kama wanamsaada!:-(

    ReplyDelete
  13. @ kaka Fadhy pole sana kwa yaliyokupata.Kaka Chib umenena.

    ReplyDelete
  14. Pole Kaka Fadhy, vitu ni matokeo, vinatafutwa, uhai katu hautafutwi, maana ni tunu aliyotupa Mungu.
    Nakupa pole tena

    ReplyDelete